BUKOBA SPORTS

Saturday, February 8, 2014

CHELSEA 3 v NEWCASTLE UNITED 0, HAT-TRICK YA EDEN HAZARD YAIPANDISHA BLUES KILELENI LEO!!

Kipindi cha kwanza kimemalizika Chelsea wakiwa 2-0, Bao zote mbili zikifungwa na Eden Hazard dakika ya 27 na 34 kipindi cha kwanza.Kipendi cha pili dakika ya 63 Chelsea wakapata mkwaju wa penati na Eden Hazard akafunga bao hilo na kutimiza bao tatu (Hat-Trick) dhidi ya timu ya Newcastle United iliyokuwa ugenini leo Stamford Bridge.Kipindi cha pili hicho hicho  Eden Hazard ametoka nje na nafasi hiyo ikachukuliwa na Andre Schürrle katika dakika ya 85. Mchezaji Moussa Sissoko  amepewa kadi ya njano katika dakika ya 90 baada ya kucheza ndivyo sivyo.
Bao hizo 3 za Eden Hazard zimehitimisha mchezo huo dakika 90 Chelsea wakiibuka shujaa kwa bao 3-0 dhidi ya Necastle United inayoshikilia nafasi ya nane kwenye msimamo wa Ligi.
Ushindi huu unaipaisha Chelsea kileleni kwa pointi 56, Arsenal wakiwa nafasi ya pili na pointi zao 55 baada ya kupokea kichapo cha bao 5-1 kutoka kwa majogoo Liverpool, Manchester City waliotoshana nguvu na Norwich ya bila kufungana kwa sare ya 0-0 wakiwa nafasi ya tatu wakiwa na pointi 54. Liverpool wanashikilia nafasi ya nne wakiwa na pointi 50.

Eden Hazard akishangilia..moja ya bao lakeEden Hazard akikimbia huku anashangilia mbele ya mashabiki wa Chelsea baada ya kufunga bao
Eden Hazard ....Hat-trick!!
Eden Hazard akifunga bao la mwisho kwa mkwaju wa penati..Frank Lampard akimbana Sammy Ameobi wa NewcastleMajanga!!! Moussa Sissoko akipagawa baada ya kuona timu yake inanyukwa bao Willian wa Chelsea akimkaba mchezaji wa Newcastle Moussa SissokoHatem Ben Arfa wa Newcastle United na Samuel Etoo kwenye  patashika!!!

MSIMAMO ULIVYO KWA SASA TIMU ZA JUU.
2013-2014 BARCLAYS PREMIER LEAGUE TABLE
OVERALLHOMEAWAY
POSTEAMPWDLFAWDLFAWDLFAGDPts
1Chelsea2517534720112028963319112756
2Arsenal251744482692122682326202255
3Manchester City2517356827110142963426184154
4Liverpool2515556330111138944425213350
























No comments:

Post a Comment