BUKOBA SPORTS

Thursday, February 6, 2014

MREMBO WEMA SEPETU APEWA UJUMBE MZITO.

WEMA Sepetu ataendelea kung’aa. Kichwa chake kinafanya kazi vizuri, anakubalika na jamii na ana uwezo mkubwa wa kufikiria. Juzi, ameachana na x boyfriend wake (yule kigogo). Amenyang’anya vitu alivyompa, wengi walifikiri kwamba ANGEKWISHA!

Kitendo cha kuendelea na ndoto zake, kufunga safari hadi Arusha na kufanya shoo Triple A Club, ni ujasiri mkubwa sana. Bado ana nafasi ya kutafuta vya kwake na akapata fedha nyingi! Wema anaweza kutumia vipaji vyake na kuwa bilionea bila kutegemea msaada wa mwanaume. Nampongeza sana kwa hilo. Wema unaweza. Simama, endelea mbele. Hongera sana kwa hilo. Imeandikwa na Joseph Shaluwa

No comments:

Post a Comment