Mashabiki hao ambao juzi kwenye mechi dhidi ya Manchester City walikuwa wakimtukana Moyes pamoja na kocha wa zamani wa klabu hiyo Sir Alex Ferguson na hata kufikia hatua ya kutaka kulishusha bango la kumsifu Moyes liliopo kwenye jukwaa la Stretford End – wanasema wanataka kuonyesha namna walivyochoshwa na kocha huyo.
Bango hilo la 'The Chosen One' limewekwa na Kundi maarufu la Washabiki wa Man United wanaokaa Jukwaa la Stretford End na wenyewe hujiita, Stretford End Flags, likiwa kama utambuzi wa chaguo la Meneja Mstaafu Sir Alex Ferguson kumteua David Moyes kumrithi.
Mara baada ya Mechi na City kumalizika, Walinzi wa Uwanja wa Old Trafford ilibidi wakae kulinda Bango hilo lising’olewe.
WAKATI HUO HUO, Kundi rasmi la Washabiki wa Man United, Manchester United Supporters Trust (MUST), limeanika rasmi mawazo yao kuhusu hali ya sasa ya Washabiki na pia kuhusu David Moyes na Timu.
MUST, kupitia Msemaji wao Sean Bones, wamesema: “Ikiwa akili yako kwa Miaka 20 mfululizo imezoea ushindi tu na ghafla hupati tena, ni lazima utaathirika kiakili!”
Hata hivyo, MUST inaamini matatizo yote si kwa sababu ya Meneja pekee.
MUST inaamini kutowekeza kwa Wamiliki wa Klabu, Familia ya Glazer, tangu wainunue Man United Mwaka 2005, ndio kitu kikubwa kimesababisha kwa Man United kushindwa vibaya Msimu huu.
MUST wanaamini kugoma kwa Familia ya Glazer kushindana na Timu kama Man City katika Soko la Uhamisho kumewaacha dhaifu katika kugombea Ubingwa.
No comments:
Post a Comment