BUKOBA SPORTS

Wednesday, March 26, 2014

BUNDESLIGA: BAYERN MUNICH WATANGAZA UBINGWA WAKIWA NA MECHI 7 MKONONI BAADA YA KUICHAPA BAO 3-1 HERTHA BERLIN.

Bayern Munich wametwaa Ubingwa wa Bundesliga kwa mara ya 24 huku wakiwa na Mechi 7 mkononi baada ya kuifunga Ugenini Hertha Berlin Bao 3-1. 
Huu ni Msimu wa kwanza wa Kocha wao Pep Guardiola ambae hajafungwa hata Mechi moja ya Bundesliga.
Katika Mechi nyingine iliyochezwa Usiku huu, Timu zilizo Nafasi za Pili na Tatu, Borussia Dortmund na Schalke 04 zilipambana na kutoka Sare ya 0-0.
Bao za Bayern katika Mechi hii na Hertha Berlin zilifungwa na Toni Kroos, Dakika ya 6, Mario Goetze, Dakika ya 14, na Franck Ribery, Dakika ya 79 huku Bao la Hertha Berlin likifungwa kwa Penati ya Dakika ya 66 iliyopigwa na Adrian Ramos.Mashabiki wa Bayern Munich wakishangilia Ubingwa wao tena wa Bundesliga huku timu yao ikiwa na mechi 7 mkononi tofauti na msimu uliopita.
Thomas Muller alijichanganya na wenzake hapa kushangilia ubingwa huo!
Wachezaji wa Bayern Munich wakipeta na kufurahia Ubingwa wao huku wakiwa mpaka sasa hawajafungwa na timu yoyote katika mechi za hivi karibuni.
Guardiola akipongezana na mwenzake

MSIMAMO TIMU TATU ZA JUU:
NA
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
1
Bayern Munich
27
25
2
0
79
13
68
77
2
BV Borussia Dortmund
27
16
4
7
59
29
30
52
3
Schalke 04
27
15
6
6
51
37
14
51

Katika Mechi nyingine iliyochezwa Usiku huu, Timu zilizo Nafasi za Pili na Tatu, Borussia Dortmund na Schalke 04 zilipambana na kutoka Sare ya 0-0.Marco Reus chupuchupu afunge bao!

BUNDESLIGA
RATIBA/MATOKEO:
Jumanne Machi 25
BV Borussia Dortmund 0 v Schalke 0
Hertha Berlin 1 v Bayern Munich 3
SV Werder Bremen 1 v VfL Wolfsburg 3
Eintr. Braunschweig 3 v FSV Mainz 1

Jumatano Machi 26
Hamburger SV v SC Freiburg
FC Nuremberg v VfB Stuttgart
Eintracht Frankfurt v Borussia Mönchengladbach
TSG Hoffenheim v Hannover 96

No comments:

Post a Comment