Bao mbili za Edin Dzeko, la kwanza likiwa kwenye Dakika ya Kwanza tu, na jingine la Yaya Toure kwenye Dakika ya 90, limeifanya Man City itoke kidedea kwenye Dabi ya Jiji la Manchester na kuitwanga Man United Bao 3-0 Uwanjani Old Trafford.
Matokeo haya, kwa mara nyingine tena, yamedhihirisha udhaifu mkubwa wa Man United Msimu huu chini ya Meneja wao alieanza Msimu huu, David Moyes, na sasa wana kazi kubwa ya kujenga upya Timu yao.
Ushindi huu umeipandisha City hadi Nafasi ya Pili wakiwa Pointi 3 nyuma ya Vinara Chelsea lakini City wana Mechi 2 mkononi na hii ni habaro njema Mashabiki wa Man City.
Dakika ya 1 Edin Dzeko anaipachikia bao la haraka City na kufanya 1-0 dhidi ya wenyeji United baada ya piga nikupige kwenye lango la Manchester United.
Wachezaji wa City wakipongezana baada ya kupata bao la haraka dakika ya kwanza.
Mapumziko Man City ndio wameenda wakiwa mbele ya bao 1-0 lililofungwa na Dzeko.
Kipindi cha pili dakika 56 City wanapata bao la pili kupitia kwa Edin Dzeko baada ya kupigwa kona na Samir Nasri na kuunganisha moja kwa moja kwa mguu.
Dakika ya 90 Yaya Toure anawapachikia bao City nakufanya 3-0
Kocha wa Manchester United akitoa maelekezo kwa wachezaji wake usiku huu wakati wanapambana na Manchester City.
Patashika kuutafuta mpira!
Kama kawaida mzee Ferg nae alikuwepo ndani ya Old Trafford!!
Aaaaaaaah tena!!! nimekuletea!
No comments:
Post a Comment