BUKOBA SPORTS

Saturday, March 29, 2014

HAPPY BIRTHDAY BISHOP METHODIUS KILAINI.

LEO tarehe 30 Machi, 2014 ukifikisha miaka 66 tangia kuzaliwa kwako. Na kwa kuwa wewe ni Kiongozi wetu wa Dini nchi yetu adhimu ya Tanzania. Nchi yenye Amani, Upendo na mshikamano kwa Wananchi wake.

Askofu Method Kilaini (amezaliwa Katoma Bukoba 30 Machi 1948) ni Askofu wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania. Aliwekwa wakfu na kardinali Agnelo Rossi mwaka 2000. Tangu hapo hadi 2009 alikuwa askofu msaidizi wa jimbo kuu la Dar es Salaam, halafu akahamishwa kuwa askofu msaidizi wa askofu wa Jimbo la Bukoba.

Askofu Kilaini alipewa upadrisho Roma mwaka 1972 na Kardinali Angelo Rossi baada ya kupata shahada ya pili ya Teologia jijini Roma. Baada ya kurudi nyumbani Bukoba Tanzania alifanya kazi parokiani, baadaye alikuwa mhazini msaidizi wa jimbo. Kati ya mwaka 1978 hadi 1985 alifundisha Historia ya Kanisa katika Seminari Kuu ya Ntungamo. Mwaka 1985 alirudi Roma na kupata shahada ya udaktari wa tauhidi katika Historia ya Kanisa kutoka chuo Kikuu cha Gregoriani mwaka 1990. Mwaka 1990 hadi 2000 alikuwa Katibu mkuu wa baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania. Kuanzia mwaka 2000 alikuwa askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam hadi mwaka 2009 alipoteuliwa kuwa askofu msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba.

Tunakutakia fanaka na furaha tele kwenye siku yako ya kuzaliwa.


Tunakutakia afya njema , Hekima na busara katika kuiongoza nchi yetu. Ili Tanzania pawe mahali bora pa kuishi.Happy birthday Bishop Methodius Kilaini Mungu akubariki sana !
Amen.

www.bukobasports.com

No comments:

Post a Comment