
Baada ya kusubiriwa kwa kipindi kirefu, hatimaye tamasha kubwa la Tubonge liloandaliwa na msanii nguli wa muziki kutoka nchini Uganda, Dr.Jose Chameleone limeacha historia hapo jana katika viwanja vya ‘Lugogo Cricket Oval’ na kuhudhuriwa na umati wa watu licha ya mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha .

Msanii kutoka Tanzania, Khaleed Mohamed ‘ T.I.D Mnyama’ alikuwa miongoni mwa wageni walihudhuria tamasha hilo kubwa ambalo pia liliwapa nafasi wasanii nchini humo kukonga nyoyo za mashabiki akiwemo Bobi Wine, kaka wa Chameleone, Ak47, kundi la GoodLyfe linaloundwa na Weasle na Radio, David Lutaalo, Xess Kayemba, Kenzo na wasanii chipukizi waliopo kwenye lebo yake ya Leone Island, Diziza, Diziza VIP na wengine kibao .

Pichani ni Jose Chameleone na TID Mnyama kabla ya kuanza kwa tamasha.


Dr.Jose Chameleone akiteta jambo na mtaalamu wa masuala ya sauti, Ras Grace .






No comments:
Post a Comment