Villa ndio waliotangulia kupata Bao kati Dakika ya 13 baada ya Frikiki ya Westwood kumshinda nguvu Kipa De Gea lakini Wayne Rooney akaifungia Man United Bao 2 moja likiwa Penati iliyotolewa baada ya Juan Mata kuangushwa ndani ya Boksi.
Juan Mata aliongeza Bao la Tatu katika Kipindi cha Pili na hilo ni Bao lake la Kwanza tangu ahamie Man United Mwezi Januari kutoka Chelsea.
Bao la 4 lilifungwa na Chicharito, alietokea Benchi, baada ya kazi nzuri ya Adnan Januzaj ambae nae pia aliingizwa Kipindi cha Pili.
Dakika ya 45′ +1 kipindi cha kwanza mwishoni, Manchester United wanapata bao la pili kwa mkwaju wa penati kupitia kwa Rooney baada ya Mata kuangushwa kwenye eneo hatari la penati na kufanya 2-1 dhidi ya Aston Villa.
Mpira ni mapumziko United wanaenda wakiwa mbele ya bao 2-1 kwenye uwanja wao Old Trafford. Dakika ya 57 Kipindi cha pili Manchester United walipata bao la tatu kupitia kwa Juan Mata baada ya piga nikupige kati ya Fellaini na wachezaji mabeki wa Aston Villa na Juan Mata kupiga na kumfunga kipa na kuandika bao la tatu. Kwa sasa United wanaongoza bao 3-1.
Dakika ya 75 kipindi cha Pili United Walifanya mabadiliko Wayne Rooney anatoka nafasi yake inachukuliwa na Javier Hernandez.
Dakika ya 90 Chicharito aliyetokea benchi anaipachikia bao United na kufanya 4-1 dhidi ya Aston Villa Baada ya kupewa pasi na Adnan Januzaj. Mpira umemalizika United wakishanda bao 4-1 dhidi ya Aston Villa.
Kabla Mechi hii kuanza Washabiki wa Manchester United walionyesha sapoti yao kwa Meneja wao David Moyes kwa kumshangilia wakati akiingia Uwanjani kwenda kukaa kwenye Benchi kabla Mechi kuanza na kuizomeoa ile Ndege iliyopita juu ya Anga ya Old Trafford ikiburuza Bango kubwa: 'Wrong One - Moyes Out' wakati Mechi imeanza tu.
Mashabiki, hasa wale waliokwaa Jukwaa maarufu la Old Trafford liitwalo Stretford End, waliimba na kumshangilia Moyes: “One David Moyes!”.
No comments:
Post a Comment