BUKOBA SPORTS

Saturday, March 29, 2014

FULL TIME: CRYSTAL PALACE 1 v CHELSEA 0, BAO LA ZAWADI LA KAPTENI JOHN TERRY LAWANYIMA RAHA BLUES!!!


Chelsea leo wamemwaga manyanga ugenini walipocheza Ugenini na timu ya Crystal Palace. John Terry alijifunga katika dakika ya 52 na kuwapa ushindi Crystal Palace wa bao 1-0. Kipigo hicho kinaondoa Matumaini ya Chelsea kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu England yameingia dosari kubwa baada kuchapwa Bao 1-0 na Crystal Palace, Timu ambayo inapigana kujinusuru na kubakia kwenye Ligi hiyo, katika Mechi iliyochezwa Uwanja wa Selhurst Park.

Bao hilo la ushindi kwa Palace lilifungwa na Nahodha wa Chelsea, John Terry, baada kupiga Kichwa wavuni kwao wenyewe kufuatia Krosi ya Dakika ya 52 ya Joel Ward.
Mara mbili Kipa wa Palace, Julian Speroni, aliokoa toka kwa Eden Hazrd na pia John Terry alipata nafasi safi lakini Kichwa chake kilipaa.
Palace walikaribia kupata Bao la Pili lakini Shuti la Cameron Jerome lilipiga Posti.

No comments:

Post a Comment