BUKOBA SPORTS

Wednesday, March 26, 2014

MANCHESTER UNITED KUFUNGWA MARA YA 6 OLD TRAFFORD!!!, VIPIGO VYA LIVERPOOL NA MAN CITY KUMTESA DAVID MOYES!! WADAU WATAKA ALE KONA!!

Baada ya kuchapwa Bao 3-0 na Mahasimu wao wakubwa, Manchester City, Jumanne Usiku na hicho ni kipigo cha pili mfululizo kwa Man United kwenye ngome yao toka kwa Mahasimu wao baada pia kutandikwa Bao kama hizo na Liverpool Wiki moja iliyopita. 
Ushindi huo wa Man City ni wa tatu mfululizo Uwanjani Old Trafford na jinsi walivyoshinda kulionyesha wazi jinsi gani Man United, chini ya Meneja David Moyes, ilivyoporomoka kwa kipindi kifupi.Msimu huu, Man United imefungwa mara 6 Uwanjani Old Trafford kwenye Ligi ambayo wako Nafasi ya 7 lakini vipigo toka kwa Liverpool na Man City, Mahasimu wao wakubwa, ndio kumeamsha zaidi manung’uniko toka kwa Mashabiki wao wengi. 
Baadhi ya Wachambuzi wanadai kuwa Moyes amerithi Kikosi ambacho uchezaji wao umeshuka lakini wengi wanadai Meneja huyo hajui kupanga Timu na hilo limemfanya abadili Kikosi katika kila Mechi anayocheza kitu ambacho hakisaidii kabisa Uchezaji Kitimu kwani kila Siku una Timu mpya.
Wengine wanadai Moyes hana uzuri wa kuiongoza Man United lakini, Paul Scholes, Mchezaji wa zamani wa Man United, ametaka Meneja huyo apewe muda zaidi na pia asaidiwe mwishoni mwa Msimu kununua Wachezaji wapya.

No comments:

Post a Comment