BUKOBA SPORTS

Saturday, March 8, 2014

SIKU YA WANAWAKE DUNIANI 2014 KAULI MBIU IKIWA NI MSUKUMO WA MABADILIKO.


Siku ya leo Dunia inasherekea siku ya wanawake ambayo huadhimishwa kila mwaka ifikapo tarehe 8 ya mwezi wa tatu kila mwaka na kauli mbiu ya mwaka huu ni Msukumo wa mabadiliko.

Sherehe hizi huadhimishwa na mataifa mbalimbali duniani kwa lengo la kuhakikisha dunia inafahamu wajibu na mchango wa mwanamke alionao kwenye jamii ya sasa.

Siku hii inaadhimishwa wakati ambapo mataifa mengi duniani yanakabiliwa na changamoto mbalimbali kuhusu kulinda haki za wanawake huku mataifa ya Afrika ndi yakionekana kuathirika na tatizo hili.
Mataifa mengi ya Afrika zikiwemo nchi za ukanda wa Afrika mashariki zimekuwa zkiripoti unyanyasaji wa wanawake ambapo baadhi ya makabila yameendelea na mila za kukeketa wanawake jambo ambalo linapigwa vita na wanaharakati wa wanawake na Umoja wa Mataifa.Washiriki wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani wakijumuika katika burudani huku wakionesha majarida anuai ya kupinga ukatili, unyanyasaji wowote wa kijinsia kwa wanawake nchini Tanzania.

No comments:

Post a Comment