Manchester United wanapata bao kupitia kwa Phil Jones bao la kichwa baada ya Robin Van Persie kuachia shuti kali la frii kiki, Katika dakika ya 34. Phil Jones likiwa ni bao lake la tatu kwa msimu huu. Kipindi cha kwanza Man United wanaenda mapumziko wakiwa mbele ya bao 1-0 dhidi ya wenyeji West Brom.
Kipindi cha pili dakika ya 63 United wanafanya mabadiliko Robin van Persie anatoka na nafasi yake inachukuliwa na Danny Welbeck. Kipindi cha pili United wanaongeza bidii na kasi na hatimae dakika ya 65 Wayne Rooney anaipachikia bao la pili na kufanya 2-0 bao la kichwa baada ya mpira kupigwa kama kona na Rafael na Rooney kujitwisha mpira huo kiurahisi mpaka langoni mwa timu ya West Brom Albion.
Dakika za mwishoni dakika ya 82 Mchezaji wa United aliyetokea benchi na kuchukua nafasi ya Van Persie Danny Welbeck akaiongezea bao la tatu United kwa kufanya 3-0 baada ya kutanguliziwa pasi safi na Wayne Rooney.

Kocha wa Man United David Moyes akiingia uwanjani Hawthorns

Mtu kati!!

Mata akibanwa na Gareth McAuley apamojana na Youssuf Mulumbu

Phil Jones akitupia nyavuni!!

Wachezaji wa Man United wakipongezana baada ya kupata bao la kwanza...

Mashetani wekundu wakipongezana

Ushindi leo!!!

Kushinda ni raha!! David Moyes meno nje leo!

Rooney akichuana na mchezaji wa West Brom Gareth

Januzaji akifanya mambo yake...

Wayne Rooney akifunga bapo la kichwa kipindi cha pili...
VIKOSI:
West Brom: West Brom: Foster; Reid, McAuley, Olsson, Ridgewell; Yacob, Mulumbu; Amalfitano, Gera, Brunt, Anichebe
Substitutes: Morrison, Myhill, Vydra, Dawson, Sessegnon, Berahino, Koulossa
Manchester United: De Gea; Rafael, Jones, Smalling, Evra; Carrick, Fellaini; Mata, Rooney, Januzaj; van Persie
Substitutes: Giggs, Lindegaard, Vidic, Young, Welbeck, Fletcher, Kagawa
No comments:
Post a Comment