BUKOBA SPORTS

Saturday, March 8, 2014

FA CUP: ARSENAL 4 v EVERTON 1, MESUT OZIL, ARTETA NA OLIVIER GIROUD WAIPATIA USHINDI GUNNERS EMIRATES!!


Dakika ya 7 Ozil inaipachikia bao Arsenal baada ya kupata pasi kutoka kwa Santi Cazorla. Dakika ya 32 kipindi hicho hicho cha kwanza Romelu Lukaku anaisawazishia bao Everton na kufanya 1-1 dhidi ya wenyeji Arsenal baada ya kupewa mpira kutoka kwa Kevin Mirallas. Kipindi cha kwanza kinalizika kwa 1-1. Kipindi cha pili Yaya Sanogo anatoka nafasi yake inachukuliwa na Olivier Giroud. Dakika ya 68 Arsenal wanapata penati na mkwaju wa huo wa Penati unapigwa na Mikel Arteta na hatimae Gunners wanapata bao na kufanya wawe mbele ya bao 2-1 dhidi ya Everton. 
Dakika ya 83 Olivier Giroud aliyeingia kutoka benchi akaipatia bao la tatu Arsenal baada ya kupewa krosi na Bacary Sagna. Dakika chache baadae dakika ya 85 Olivier Giroud akatupia bao tena la pili akipewa pasi na fundi Mesut Özil.Mashabiki wa Everton wakishangilia....bao la kusawazisha mapema kipindi cha kwanza.Mesut Ozil akiwafunga Everton bao la mabema dakika ya sabaMpaka nyavuni............
Wachezaji wa Arsenal (kushoto) wakipongezanaMikel akichonga penati..Mikel Arteta akishangilia bao Oliver Giroud akifunga bao la tatuMcCarthy na Carzorla wakikimbilia mpiraArteta akimzuia mchezaji wa Everton..Olivier akifunga bao la nne Olivier Giroud (katikati) akishangilia bao na Ozil pembeni...Wachezaji wa Arsenal wakipongeza baada ya kufunga bao dhidi ya Everton
VIKOSI:
Arsenal: Fabianski, Sagna, Mertesacker, Vermaelen, Gibbs, Flamini, Arteta, Oxlade-Chamberlain, Ozil, Cazorla, Sanogo.
Subs: Rosicky, Podolski, Giroud, Viviano, Jenkinson, Miyaichi, Gnabry.
Everton: Robles, Coleman, Stones, Distin, Baines, McCarthy, Barry, Mirallas, Barkley, Pienaar, Lukaku.
Subs: Hibbert, McGeady, Deulofeu, Naismith, Osman, Howard, Browning.

No comments:

Post a Comment