BUKOBA SPORTS

Sunday, April 13, 2014

CASTLE LAGER YAZINDUA MASHINDANO YA PERFECT SIX KWA VYOMBO VYA HABARI

Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Fimbo Buttallah akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) katika uzinduzi wa shindano la kitaifa la mpira wa miguu litalohusisha wachezaji sita kila upande linaloitwa ‘Castle Lager Perfect Six’ uliofanyika jana jijini Dar es Salaam. Pembeni yake kushoto ni Meneja wa bia ya Castle Lager Kabula Nshimo.
Meneja wa bia ya Castle Lager Kabula Nshimo akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) katika uzinduzi wa shindano la kitaifa la mpira wa miguu litalohusisha wachezaji sita kila upande linaloitwa ‘Castle Lager Perfect Six’ uliofanyika jana jijini Dar es Salaam. Pembeni yake kulia Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Fimbo Buttallah.Wachezaji wa Timu ya Xavi (wenye jezi nyeusi) na Mascherano (wenye jezi kijivu) wakijadiliana jambo wakati wa mchezo wa tamasha la Perfect Six Media Bonanza ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa shindano hilo la kusisimua. Timu ya Xavi iliibuka kidedea kwa bao 6-1. Tamasha la Perfect Six Media Bonanza lililofanyika katika ufukwe wa Mbalamwezi jijini Dar es Salaam na lilikuwa na lengo la kuwakutanisha pamoja waandishi wa habari toka vyombo mbali mbali ikiwa ni pamoja na kuwajengea uelewa wa mchezo huo.Wachezaji wa Timu ya Xavi (jezi nyeusi) wakishambulia vikali katika lango la timu ya Puyol (jezi kijivu), ambapo katika mtangange huo Puyol waliibuka kidedea kwa kutwaa ubingwa kwa bao 5-1. Na Mascherano wao waliibuka washindi wa pili. Tamasha la Perfect Six Media Bonanza lililofanyika katika ufukwe wa Mbalamwezi jijini Dar es Salaam.Kombe na Medali zisubiri washindi.Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania, Fimbo Buttallah akimkabidhi kombe la ushindi timu kapteni wa timu ya Puyol, Majuto Omary mara baada ya kuibuka washindi wa tamasha la Perfect Six Media Bonanza lililofanyika katika ufukwe wa Mbalamwezi jijini Dar es Salaam.Wachezaji wa timu ya Puyol wakiongozwa na kapteni wao, Majuto Omary wakishangilia ushindi wao, pembeni yao ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Fimbo Buttallah (kulia) na Meneja wa bia ya Castle Lager Kabula Nshimo (kushoto).
Castle Lager kupitia ushirikiano wake na FC Barcelona leo imezindua shindano la kitaifa la mpira wa miguu litakalohusisha wachezaji sita kila upande. Shindano hilo litakalojulikana kama “Castle Lager Perfect 6” litamalizika kwa kupata washindi ambao watatembelea uwanja wa Camp Nou na kujionea FC Barcelona ikicheza katika ziara ambayo itagharamiwa kila kitu na Castle Lager.
Castle Lager ikishirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari wa Michezo (TASWA) wameandaa tamasha la Perfect Six Media Bonanza ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa shindano hili la kusisimua. Hii ni njia ya kuwaleta pamoja waandishi wa habari na kuwapa uelewa juu ya ushirikiano huu na pia ni fursa kwao wenyewe kushiriki na kujionea namna tukio hili ambalo litahusisha mamia ya Watanzania kwa muda wa miezi mitano mwaka huu linavyofanyika.
Akiongea kwenye uzinduzi jijini Dar es salaam leo, Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania, Fimbo Buttallah amesema shinano la Perfect Six limelenga kuzungumza na wanywaji wa Castle Lager ambao wana shauku ya kucheza mpira wa miguu, kuleta pamoja wanywaji wa Castle Lager kutoka baa mbalimbali ili wafurahie pamoja, kuongeza mauzo ya Castle Lager na kuwapa zawadi wateja wa bia hiyo. Katika kutambua mchango mkubwa wa vyombo vya habari, tumeamua kuzindua shindano hili na bonanza la waandishi wa habari.
“Hii itafatiwa na shindano litakalofanyika nchi nzima ambapo timu mbalimbali katika Kanda saba zitasajiliwa na kucheza katika hatua za mtoano kwenye maeneo mbalimbali ambayo yatachaguliwa na kutangazwa mapema. Kila kanda itatoa timu moja na kufanya jumla ya timu saba ambazo zitawakilisha Kanda hizo huku timu ya nane ikitoka kwenye vyombo vya habari. Timu hizo zitachuana kwa mtoano kwenye robo fainali, nusu fainali, na hatimaye fainali.
“Timu itakayoshinda itapata nafasi ya kipekee kwenda Hispania kutembelea uwanja wa Camp Nou na kujionea timu ya FC Barcelona ikicheza,” Buttallah aliongeza.
Tunachukua nafasi hii kuwahamasisha wanywaji wa Castle Lager kwamba Perfect Six itawafikia popote walipo kupitia bar mbalimbali hivyo waanze kuandaa timu zao. Vilevile tunaikaribisha timu ya waandishi wa habari itakayoshiriki ikiiwakilisha TASWA na ni matumaini yetu kwamba shindano hili litaleta msisimko mkubwa,” alisema Buttallah.

No comments:

Post a Comment