Liverpool wanaingia kwenye Mechi hii wakiwa hawajafungwa katika Mechi 14 za Ligi, wameshinda 9 kati ya hizo, wakati Man City hawajafungwa katika Mechi 10 za Ligi za Ugenini.
Kocha Brendan Rodgers kwenye mazoezi na wachezaji wake kujiweka sawa na mtanange wa leo jumapili dhidi ya City
Meneja wa Liverpool Brendan Rodgers itabidi aamue kumchezaji yupi acheze Sentahafu kati ya Mamadou Sakho na Daniel Agger baada ya wote kupona maumivu yao lakini watamkosa Jose Enrique ambae bado kaumia ila Joe Allen anaweza kuanza ikiwa Rodgers ataamua anahitaji Kiungo wa ziada kwenye safu hiyo.
Man City wao wana faraja kubwa baada ya Mfungaji wao Bora Sergio Aguero, aliekosa Mechi 5, kupona na sasa yuko fiti kwa Mechi hii.
Steven Gerrard kuendesha makali yake leo au la!
Anfield itakuwa ni Siku maalum ambapo mbali ya hii kuwa Bigi Mechi pia itakuwa ni Siku 2 tu kabla ya kuadhimisha Miaka 25 ya Maafa ya Hillsborough ambapo Mashabiki wao 96 walikufa na 766 kujeruhiwa Uwanja wa Hillsborough Aprili 15 Mwaka 1989 wakati wa Mechi ya Nusu Fainali ya FA CUP kati ya Liverpool na Nottingham Forest.
Luis Suarez na Daniel Sturridge wameishafunga bao 49 msimu huu wa Ligi
Lakini City itaendelea kumkosa Matija Nastasic ambae ana tatizo la Goti, Vincent Kompany nae jana kwenye mazoezi aliumia ni mashaka kucheza leo
Straika Sergio Aguero: Man City wao wana faraja kubwa baada ya Mfungaji wao Bora Sergio Aguero, aliekosa Mechi 5, kupona na sasa yuko fiti kwa Mechi hii.
No comments:
Post a Comment