BUKOBA SPORTS

Saturday, April 26, 2014

EPL USIKU HUU SAA 1:30, OLD TRAFFORD NI MANCHESTER UNITED vs NORWICH...MECHI YA KWANZA YA KOCHA WA MUDA RYAN GIGGS.

LEO OLD TRAFFORD, itamshuhudia Meneja wake mpya wa muda, Ryan Giggs, akiiongoza Manchester United kwa mara ya kwanza itakapopambana na Norwich City katika Mechi ya Ligi Kuu England na wakati huo huo, Sir Alex Ferguson, amesema anaamini Giggs anafaa kuwa Meneja wa kudumu wa Klabu hiyo.

Licha ya wengi kumuona Giggs, mwenye Miaka 40, kuwa hana uzoefu wa kutosha wa kuiongoza Man United baada ya kupewa Umeneja kwa muda kufuatia kufukuzwa kwa David Moyes Jumanne iliyopita, Sir Alex Ferguson, ambae ndie aliependekeza Moyes amrithi yeye baada ya kustaafu Juni Mwaka Jana, amesema Giggs anao uzoefu wa Miaka 20 na ushei hapo Manchester United.Ametamka: “Nadhani Giggs anastahili kupewa nafasi ya kudumu. Anao uzoefu wa Miaka 20 na ushei hapo Manchester United. Nilimsaini akiwa na Miaka 13 tu. Amepitia kila hali Klabuni hapo-ana uzoefu wa mafanikio, pia hali ya kupanda na kushuka. Anajua fika nini unastahili kuwa Mchezaji wa Man United na nimefurahishwa kwa yeye kuwachukua Paul Scholes na Nicky Butt..Maprofeshenali wa kweli! Wanaielewa Klabu, wachapa kazi, na ni Watu safi. Pale upo umoja mzuri, bila wasiwasi!”

No comments:

Post a Comment