Ryan Giggs, akiingia Uwanjani kabla Mechi kuanza na Wasaidizi wake, Wachezaji wenzake wa zamani Man United, Nicky Butt, Paul Scholes na Phil Neville, alipokewa kwa shangwe kubwa ya Uwanja mzima na Old Trafford ilizizima muda wote wa Mechi hii.
Wakicheza kwa ari, bidii, ufundi na presha ya mashambulizi, kama ile Manchester United ya zamani chini ya Sir Alex Ferguson, Wayne ndie aliefungua milango kwa Bao la Penati ya Kipindi cha Kwanza iliyotolewa na Refa Lee Probert baada ya Danny Welbeck kuangushwa na Whittaker.
Alikuwa Rooney tena aliepachika Bao la Pili mapema mara baada Kipindi cha Pili kuanza kwa Bao la kifundi.
Juan Mata, alieingizwa Kipindi cha Pili kumbadili Danny Welbeck katika Dakika ya 60, ndie aliefunga Bao 2 nyingine.Kipigo hiki kimewaacha Norwich wakiwa Pointi 1 tu juu zile Timu 3 za mkiani ambazo ziko hatarini kushuka Daraja.
Kocha Ryan Giggs
Giggs kama Ferg!!! Muda!!!
No comments:
Post a Comment