Dakika ya 19 mchezaji wa Sheff United Jose Baxter anaipatia bao la kwanza timu yake baada ya kupata Krosi safi kutoka kwa John Brayford. Dakika ya42′ Y. Sagbo Aliipatia bao la kusawazisha timu yake Hull City lakini bao hilo halikuweza kudumu nao Sheff United waliongeza bao la pili na kufanya 2-1 dhidi ya Hull kwenye dakika ya 44. Kipindi cha pili dakika ya 49 Matt Fryatt aliisawazishia bao Hull City nakufanya 2-2. Dakika ya 54 Hull City wanaongeza bao la tatu kupitia kwa Tom Huddlestone baada ya kupata pasi kutoka kwa David Meyler. Dakika ya 67 Stephen Quinn anaipachikia bao la nne Hull City. Dakika za lala salama dakika ya 90 Sheff United walipata bao kupitia kwa Jamie Murphy. Dakika ya 90 hapo hapo kwenye dakika za nyongeza Hull waliongeza bao na mtanange kumalizika kwa bao 5-3.Hull City wanasonga hatua ya nusu fainali na watakutana na Arsenal.
No comments:
Post a Comment