
Baada ya kutolewa kwenye Capital One Cup, kutupwa nje ya UEFA CHAMPIONS na pia kufungwa 3-0 hivi Juzi na Everton na kumaliza kabisa matumaini yao ya Ubingwa na kuhatarisha nafasi yao ya kumaliza 4 Bora Msimu huu, Arsenal wamebakiwa na nafasi moja tu kutwaa Kombe Msimu huu.
Lakini Arsenal wanawavaa Mabingwa Watetezi wa FA CUP, Wigan Athletic, ambao Siku 3 tu baada kutwaa Kombe hilo Msimu uliopita walishuka Daraja kutoka Ligi Kuu England na kwenda kucheza Daraja la chini, Championship.
Licha ya kuwa Daraja la chini, Wigan wametetea vyema Kombe lao Msimu huu na Raundi iliyopita waliwafunga Manchester City Bao 2-1 ikiwa ni Marudio ya Fainali yao ya Mwaka Jana ambapo Wigan waliwatoa Man City na kutwaa Kombe hili.
Kombe la mwisho kwa Arsenal kuchukua ilikuwa ni FA CUP waka 2005 walipowatoa Man United kwa Mikwaju ya Penati Tano Tano.
Nusu Fainali nyingine ya FA CUP itachezwa Jumapili Aprili 13 Uwanjani Wembley kati ya Hull City na Sheffield United ambayo ipo Daraja la Ligi 1.
Fainali ya FA CUP itachezwa Mei 17.
VIKOSI VINAWEZA KUWA HIVI:
Wigan Athletic: Al Habsi; Beausejour, Barnett, Boyce, Ramis, Perch; Gomez, Mcechran, McArthur, McManaman; Powell.
Arsenal : Fabianski; Sagna, Mertesacker, Vermalen, Gibbs; Kallstrom, Arteta; Chamberlain, Cazorla, Podolski, Sanogo.
RATIBA: FA CUP
Nusu Fainali
Mechi zote kuchezwa Wembley Stadium
Jumamosi Aprili 12
Wigan v Arsenal
Jumapili Aprili 13
Hull City v Sheffield United
No comments:
Post a Comment