Jana, Meneja wa Timu, David Moyes, alidokeza kuwa mwishoni mwa Msimu wataijenga upya Timu na wapo Wachezaji ambao washawasuka ili kuhamia Old Trafford.
Uamuzi huu unamaanisha kuwa wapo Wachezaji kadhaa itabidi wauzwe ili wapya waje.
Fletcher amefafanua: “Wachezaji ni lazima wacheze vizuri ili wabaki kwenye mipango ya Meneja. Ipo minong’ono mingi kuwa yatakuwepo mabadiliko makubwa!”
Wachambuzi wamedai Moyes atalazimika kusaini Wachezaji kadhaa wapya wakiwemo, Sentahafu, Mafulbeki wawili na Viungo wawili ili kuimarisha Timu na kuanza kuijenga upya.
Akigusia uwezekano wa kukosa kucheza UEFA CHAMPIONS LIGI kwa mara ya kwanza tangu Mwaka 1995, Fletcher alisema: “Hatutafikiria hilo, tutafikiria kutwaa Ubingwa na kurudi Ulaya kama Mabingwa!”
Kuhusu uwezekano wa wao kucheza EUROPA LIGI Msimu ujao, Fletcher alisema: “Tuikumbatie! Twende na kutwaa Kombe!”
No comments:
Post a Comment