BUKOBA SPORTS

Tuesday, April 22, 2014

FULL TIME, EPL- MANCHESTER CITY 3 vs WEST BROM 1, CITY WAZIDI KUJIKONGOJA TARATIBU!!

Back on track: Manchester City defeated West Brom at the Etihad to get back to winning ways
BAO tatu zilizofungwa na Pablo Zabaleta mapema dakika ya 3, Bao la pili likifungwa na Sergio Agüero katika dakika ya 10 huku Martín Demichelis akimaliza bao la tatu dakika ya 36 zimewapa ushindi leo wa 3-1 wakiwa kwao kwenye uwanja wao wa Etihad.
Bao la kufutia machozi kwa upande wa West Brom limefungwa na Graham Dorrans katika dakika ya 16 kipindi cha kwanza.
Kipindi cha pili hakuna timu iliyoweza kuziona nyavu za mwenzake licha ya timu zote kushambuliana.

Hadi Mapumziko Bao zilikuwa Man City 3 WBA 1.
Kwa matokeo haya, City imebaki Nafasi ya 3 ikiwa Pointi 1 nyuma ya Chelsea na Pointi 6 nyuma ya Vinara Liverpool huku wakiwa na Mechi 1 mkononi.

Pablo Zabaleta akiifungia bao la mapema City kwenye uwanja wao Etihad, Dakika ya tatu bao!!

Zabaleta alitupia kwa kichwa baada ya kuona nafasi iliyoachwa na kipa wa West Brom Ben Foster

Akishangilia bao lake

Sergio Aguero alifunga bao la pili  na kufanya 2-0 katika dakika ya 10

Aguero akimfunga  Foster

Aguero na Fernandinho wakipeana tano!!!!!!!!!David Silva aliumia kipindi cha pili.

No comments:

Post a Comment