LEO Jumanne, ndani ya Estadio Vicente Calderon, Vinara wa La Liga, Atletico Madrid, wataikaribisha Chelsea ya Engand.
Siku ya Pili yake, yaani Jumatano Usiku, huko Santiago Bernabaeu, Real Madrid watakuwa Wenyeji wa Mabingwa Watetezi wa UCL, Bayern Munich.
ATLETICO MADRID v CHELSEA:
Jose Mourinho ameshawahi kuifikisha Chelsea mara 2 Nusu Fainali ya UCL, Mwaka 2005 na 2007, na kutolewa na Liverpool.

Lakini safari hii wapo Uwanja wa Vicente Calderon ambao Atletico Madrid hawajafungwa hata Mechi moja ya La Liga Msimu huu na wanaongoza Ligi hiyo ya Spain wakiwa Pointi 4 mbele ya Barcelona.
Chelsea watatinga kwenye Mechi hii bila ya Fulbeki wao Branislav Ivanovic ambae amefungiwa na hili linaweza kumrudisha Kikosini Mkongwe Ashley Cole ambae amepoteza namba kwa Cesar Azpilicueta ambae atapelekwa Fulbeki ya Kulia na Cole kucheza kushoto.
Pia Chelsea inaweza kumkosa Eden Hazard ambae ni Majeruhi pamoja na Nemanja Matic na Mohamed Salah ambao hawaruhisiwi na UEFA kuichezea Chelsea kwenye Mashindano haya.
Kwa Atletico, chini ya Kocha Diego Simeone, hawana matatizo kwenye Kikosi chao na hata Kipa wao, Thibaut Courtois, ambae yuko hapo kwa Mkopo kwa Misimu mitatu sasa akitokea Chelsea, ameruhusiwa kuichezea Atletico na UEFA baada ya kuibuka utata kwamba Mkataba wake haumruhusu kucheza Mechi dhidi ya Chelsea.
UEFA CHAMPIONS LIGI
NUSU FAINALI: RATIBA
Jumanne Aprili 22
Atletico Madrid v Chelsea
Jumatano Aprili 23
Real Madrid v Bayern Munich
MARUDIANO:
Jumanne Aprili 29
Bayern Munich v Real Madrid
Jumatano Aprili 30
Chelsea v Atletico Madrid
FAINALI: Estádio da Luz, Lisbon, Portugal 24 Mei 2014.
Siku ya Pili yake, yaani Jumatano Usiku, huko Santiago Bernabaeu, Real Madrid watakuwa Wenyeji wa Mabingwa Watetezi wa UCL, Bayern Munich.
ATLETICO MADRID v CHELSEA:
Jose Mourinho ameshawahi kuifikisha Chelsea mara 2 Nusu Fainali ya UCL, Mwaka 2005 na 2007, na kutolewa na Liverpool.
Lakini safari hii wapo Uwanja wa Vicente Calderon ambao Atletico Madrid hawajafungwa hata Mechi moja ya La Liga Msimu huu na wanaongoza Ligi hiyo ya Spain wakiwa Pointi 4 mbele ya Barcelona.
Chelsea watatinga kwenye Mechi hii bila ya Fulbeki wao Branislav Ivanovic ambae amefungiwa na hili linaweza kumrudisha Kikosini Mkongwe Ashley Cole ambae amepoteza namba kwa Cesar Azpilicueta ambae atapelekwa Fulbeki ya Kulia na Cole kucheza kushoto.
UEFA CHAMPIONS LIGI
NUSU FAINALI: RATIBA
Jumanne Aprili 22
Atletico Madrid v Chelsea
Jumatano Aprili 23
Real Madrid v Bayern Munich
MARUDIANO:
Jumanne Aprili 29
Bayern Munich v Real Madrid
Jumatano Aprili 30
Chelsea v Atletico Madrid
FAINALI: Estádio da Luz, Lisbon, Portugal 24 Mei 2014.
No comments:
Post a Comment