BUKOBA SPORTS

Tuesday, April 22, 2014

DAVID MOYES KIBARUA CHAKE CHAOTA NYASI!!! KLABU YA MAN UNITED YATHIBITISHA KUMTIMUA KAZI MOYES. RYAN GIGGS KUSHIKA HATAMU MPAKA MWISHO WA MSIMU!!


Hatimaye kocha Manchester United David Moyes amefukuzwa kazi, miezi 10 baada ya kumrithi Sir Alex Ferguson.
United jana waligoma kuthibitisha kuhusu ripoti kwamba Moyes angefukuzwa mwishoni mwa msimu.
Moyes, 50, alichaguliwa na Sir Alex Ferguson kumrithi wakati kocha huyo mwenye 72, alipoamua kustaafu baada ya miaka 26 mwaka jana baada ya ligi kuisha.
Moyes aliondoka Everton na kusaini mkataba wa miaka sita na mabingwa ya Premier league.
Kwenye taarifa rasmi, klabu ilisema: “Tungependa kumshukuru kwa kazi nzuri aliyoifanya, uaminifu wake aliokuwa nao kwenye kazi yake”.
Ryan Giggs kwa pamoja na Nicky Butt watashika majukumu ya ukocha mpaka mwishoni mwa msimu.

Mashabiki wa United wakiwa wachache Uwanjani wakati wa malumbano ya hapa na pale kabla ya mtanange huku wakishinikiza baongo la  'Chosen One' kuondolewa uwanjani hapo..

Moyes akiwa amebeba kombe la Ngao ya Jamii (Community Shield) baada ya Man  United kuifunga Wigan bao 2-0 kwenye uwanja wa  Wembley mwezi wa Nane kipindi cha nyuma.

United walishinda 4-1 dhidi ya Swansea City kwenye mtanange wao wa kwanza...na Hapa ndipo Kocha huyo alianzia furaha yake.

Kocha Moyes akisalimia mashabi wake kwenye uwanja wa Old Trafford kwenye mechi dhidi yake na Chelsea.
Moyes alifungwa uwanjani  Anfield  Daniel Sturridge kwa bao l na  Liverpool mwezi septemba

Moyes akiwaongoza wachezaji wake wa United kwenye kiwanja cha mazoezi cha Carrington kujiandaa na mechi za UEFA mwezi huo huo wa septemba.
United walichapwa na Bayer Leverkusen 4-2 kwenye uwanja wa  Old Trafford kwenye UEFA

Kibano cha 4-1 kutoka kwa Manchester City mwezi Septemba 24, Kilikuwa kibano kibaya sana kwake!!!
Man United walitolewa na Liverpool kwenye kombe la Capital One Cup hatua ya mzunguko wa tatu tu.
Moyes akishangilia bao la Javier Hernandez, United walipoichapa Stoke City bao 3-2 nyumbani Old Trafford
 Moyes sits and considers his options as United lose 1-0 to his former club Everton on December 4

Moyes na majanga yake mbele ya mchezaji Hatem Ben Arfa huku kocha Alan Pardew mwezi Disemba walipomchapa bao 1-0 kutoka kwa Newcastle United

 Moyes alikuwa akiukimbilia mpira kwenye mstari walipochapwa na  Tottenham

Moyes akilalamika juu ya jambo la kuushika mkono mpira kwenye mtanange na Tottenham ambapo hakuona lolote lililochukuliwa na waamuzi wa soka.

Moyes tena alifungwa bao 2-1 na Sunderland  kwenye Capital One Cup nusu fainali.

Phil Neville akiwa na kiongozi wake Moyes wakati walipotolewa na Sunderland kwenye matuta

 Moyes alimnunua Juan Mata kutoka Chelsea kwa £37m

United pamoja na usajili walifungwa bao 2-0 kutoka kwa Olympiacos hatua ya 16 Champions Ligi.

Lakini Hat -trick ya Robin van Persie iliwapa matumaini ya kuendelea kwenye marudiano walipoifunga timu hiyo bao  3-0 win kwenye uwanja wa  Old Trafford na kwenda kukutana na  Bayern Munich ambao waliwafunga na kuwatoa.
Chini ya David Moyes United wamekuwa chini mno kisoka..

Shabiki akimyooshea kidole kocha David Moyes wakati wa kibano cha bao 3-0 kutoka kwa Manchester City
Askari wakililinda bango la "The Chosen One" Old Trafford

Ndege nayo ilishinikiza kuondoka kwa David Moyes dhidi ya mtanange kati ya United na Aston Villa.

United walitoka sare ya 1-1 nyumbani na Bayern Munic
Bayern waliichapa bao 3-1 na kuitoa nje ya mashindano United ya Champions League
Kipigo: kutoka kwa Everton cha bao 2-0 kilionesha Moyes kwamba ni dalili tosha kuwaaga mashabiki wake!

No comments:

Post a Comment