Akihojiwa na Wanahabari, Hodgson amesema tayari ana mipango thabiti kabla hajatangaza Kikosi chake cha Wachezaji 23 hapo Mei 13 na uchaguzi wake huo wa Wachezaji unazingatia fomu ya Mchezaji ya Miezi kadhaa na hata Miaka.
Amesema: “Hakuna kitu kitakachotokea Gemu hizi 4 za mwisho na Mchezaji kung’ara na kunibadilisha mimi. Siwapimi Wachezaji kwa hali zao za Dakika za mwisho kwenye Mechi 2 au 3! Napima Wachezaji kwa zaidi ya Miaka miwili. Na kama yuko mpya kaibuka basi nampima kwa Miezi kadhaa. Siwezi kufanya uamuzi kwa kutazama Wiki iliyopita tu na hii ni mbaya sana kupima vipaji!”
Aliongeza: “Nilishakuwa na fikra za wazi nini nataka kufanya na Kikosi hiki kwa muda mrefu sana. Hivi sasa najua wazi nini nataka kufanya na hii Timu.”
Hodgson ndie Meneja wa kwanza wa Kiingereza kuiongoza England kwenye Fainali ya Kombe la Dunia kwa Miaka 16 baada kuongozwa na Wageni kina Sven-Göran Eriksson, kutoka Sweden, kwenye Fainali za Kombe la Dunia Mwaka 2006 na kutolewa Robo Fainali, na kisha Fabio Capello wa Italy kwenye Fainali za Mwaka 2010 na kubwagwa nje Raundi ya Pili.
England, ambao wako Kundi D huko Brazil, wataanza Kampeni yao dhidi ya Italy hapo Juni 14 Mjini Manaus na kufuatia Mechi dhidi ya Uruguay na Costa Rica.
No comments:
Post a Comment