Stamford Bridge, London, England
LEO JUMATANO Usiku Stamford Bridge itazizima kwa Mechi hii kubwa ya Marudiano ya Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI ambayo Wenyeji Chelsea watatinga wakitokea kwenye ushindi mkubwa wa Jumapili huko Anfield walipowatwanga Vinara wa Ligi Kuu England Liverpool Bao 2-0 huku wakichezesha Kikosi dhaifu.
Chelsea wameshinda mara 1 tu kati ya 4 walizokutana Nusu Fainali na Klabu toka Spain na hiyo moja ilikuwa dhidi ya Barcelona Msimu wa 2011/12. Mwaka 2009 walitolewa na Barcelona, 1998/99 walitolewa na RCD Mallorca kwenye Kombe la Washindi la UEFA na 1994/95, walibwagwa na Real Zaragoza.
Timu hizi zinatinga kwenye Mechi hii zikiwa suluhu baada kutoka Sare ya 0-0 huko Estadio Vicente Calderon Wiki iliyopita Matokeo ambayo yanawalazimu Chelsea kushinda Mechi hii ikiwa watataka kutinga Fainali.
Kwa Atletico, Sare yeyote ya Magoli ni ushindi kwao maana watakuwa wamefunga Goli za Ugenini.
Lakini Chelsea wanaingia kwenye Mechi hii wakiwa na habari njema kufuatia kupona kwa Wachezaji wao Nahodha John Terry, Kipa Petr Cech, ambao waliumia walipocheza na Atletico Wiki iliyopita, na Straika Samuel Eto’o, ambae hakucheza Mechi hiyo ya Wiki iliyopita.
Wachezaji hao wote Leo walijumuika Mazoezini na wenzao.
Wachezaji watakaokosena kutokana na Kifungo cha Mechi 1:
-Chelsea itawakosa Frank Lampard na John Mikel Obi
-Atletico watamkosa Gabi
Uso kwa Uso
Mara ya mwisho kwa Chelsea na Atletico kukutana ni kwenye UEFA Super Cup Mwaka 2012 ambapo Radamel Falcao alipiga Hetitriki katika Kipindi cha Kwanza na kuipa Atletico ushindi wa Bao 4-1 huku Bao la 4 likifungwa na Miranda na Bao la Chelsea kufungwa na Garry Cahill.
-Mara nyingine pekee kwa Chelsea na Atletico kukutana ni kwenye Kundi D la UEFA CHAMPIONS LIGI Msimu wa 2009/10 ambapo Chelsea, chini ya Carlo Ancelotti, walizoa Pointi 4 kwa kuichapa Atletico 4-0 Uwanjani Stamford Bridge na kutoka Sare 2-2 huko Madrid na kufuzu kama Vinara wa Kundi D huku Atletico wakimaliza Nafasi ya 3.
DONDOO MUHIMU:
-FAINALI: Estádio da Luz, Lisbon, Portugal 24 Mei 2014
Bayern Munich/Real Madrid v Chelsea/Atletico Madrid
Na leo hii tena kazi ipo
-FAINALI: Estádio da Luz, Lisbon, Portugal 24 Mei 2014
Bayern Munich/Real Madrid v Chelsea/Atletico Madrid
No comments:
Post a Comment