BUKOBA SPORTS

Tuesday, April 1, 2014

KOMBE LA DUNIA: WIMBO RASMI KUPIGWA NA SANTANA, WYCLEF, AVICII, ALEXANDRE PIRES!!


WIMBO WENYEWE
UNAITWA Dar um Jeito (We Will Find A Way)!

FIFA na Sony Music Entertainment zimetangaza kuwa Wimbo Rasmi wa Fainali za Kombe la Dunia za huko Brazil 2014 ambao unaitwa “Dar um Jeito (We Will Find A Way)”, utapigwa kwenye Sherehe za Kufunga Mashindano hayo huko Rio de Janeiro hapo Juilai 13 ukishirikisha Mastaa Carlos Santana, Wyclef, Avicii na Alexandre Pires.Huu ni Wimbo wa nne kwa ajili ya Fainali hizo zitakazoanza Juni 12 Nchini Brazil nyingine zikiwa ule Wimbo Rasmi wa Pitbull, Jennifer Lopez na Claudia Leitte, mwingine ni SuperSong uliorekodiwa na Ricky Martin na ule rasmi wa Kinyago Maalum [Official Mascot] uliotolewa Mwaka 2012 na Mwimbaji wa Brazil Arlindo Cruz.
Akiongea kuhusu Wimbo Dar um Jeito (We Will Find A Way)”, Mkurugenzi wa Masoko wa FIFA, Thierry Weil, amesema ni kitu kikubwa kwa Mastaa wakubwa Duniani kushirikiana na kutoa kipande kizuri mno.
Nae Carlos Santana, Gwiji la kucharaza Gitaa, akizungumzia Wimbo huo amesema: “Ni heshima kubwa kushiriki kwenye Fainali za FIFA za Kombe la Dunia na kuufanya Wimbo “Dar um Jeito (We Will Find A Way”) kuwa Wimbo Rasmi. Pamoja na Ndugu zangu, Wyclef, Avicii na Alexandre Pires, tunangoja kwa hamu kuupiga huko Rio de Janeiro Mwezi Julai!”

Mbali ya Mastaa hao wakubwa kushiriki kwenye Wimbo huo, pia Watengenezaji wakubwa wameshiriki akiwemo Ash Pournouri, ambae amewahi kuteuliwa kwenye Tuzo za Grammy mara mbili.

Pournouri amesema: “Kwa Kireno, ‘Dar Um Jeito’ maana yake ni kutafuta njia kuvishinda vikwazo na vitu vinavyozuia!”

No comments:

Post a Comment