BUKOBA SPORTS

Thursday, April 3, 2014

RUVU SHOOTING YAIPANIA AZAM, WAPANGA KUITIBULIA NA KUIKWAMISHA AZAM KILELENI!

Na Faustine Ruta, Bukoba
MCHEZO wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Azam FC na wenyeji Ruvu Shooting uliokuwa ufanyike Aprili 6, mwaka huu Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani umesogezwa mbele hadi Aprili 9, imefahamika.
Klabu hiyo ya rvu Shooting imetamba kuwang'oa  vinara wa Ligi kuu Vodacom Bara, Timu ya AZAM Fc kwa jembe la mkono baada ya magreda kushindwa na kuharibu shangwe zao za kuanza kushangilia Ubingwa. Bwire amesema kwa upande wa wachezaji majeruhi alisema Ibrahim Suzan bado hali yake si nzuri lakini Elius Maguli na Ayoub Kitala walikosa mechi ya dhidi ya Kagera Sugar kutokana na kuwa na kadi za njano tatu na katika mechi hiyo ya Azam watakuwepo na watacheza. Ruvu Shooting mpaka sasa katika msimamo wa Ligi kuu Bara ipo katika nafasi ya sita wakiwa na pointi 32 huku Azam ikiwa Kileleni na pointi zao 53 ikifuatiwa na Yanga yenye pointi 46 na mbeya City ni ya tatu ikiwa na point 45.

Ruvu Shooting kwenye msimamo wapo nafasi ya 6 wakiwa na pointi 32
Wachezaji wa Ruvu Shooting wakifanya mazoezi hivi karibuni

No comments:

Post a Comment