Timu nzima ya Kampuni ya Proin Promotions Limited imeondoka leo jijini Dar Es Salaam kuelekea Mkoani Mwanza kwaajili ya kuendesha Shindano la Kusaka Vipaji vya Uigizaji Tanzania ambapo Kwa kuanza shindano hili litaanzia Mkoani Mwanza Katika Kanda ya Ziwa.
Usaili wa Kutafuta vipaji utafanyika mnamo tarehe 5 mwezi huu katika ukumbi wa Isamilo lodge ambapo vijana wengi wanaomba kuhudhuria kwa wingi ili kuweza kuonyesha vipaji vyao.
Zoezi la kusaka Vipaji katika Kanda ya ziwa utafanyika kwa Siku nne kuanzia tarehe 5 mwezi huu na pia kwa kanda ya Ziwa Usaili utafanyika katika Mikoa Miwili ya Kigoma na Mwanza.
Proin Promotions Limited imeamua kusaka vipaji ili kuweza kuinua tasnia ya filamu nchini.
No comments:
Post a Comment