BUKOBA SPORTS

Friday, April 11, 2014

SIMBA, ASHANTI UTD KUVAANA TAIFA

Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaendelea (Aprili 12 mwaka huu) katika raundi ya 25 ambapo Tanzania Prisons itaivaa Rhino Rangers (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, jijini Mbeya) wakati Coastal Union itakuwa mwenyeji wa JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Kesho kutwa (Aprili 13 mwaka huu) kutakuwa na mechi nyingine tano za kukamilisha raundi hiyo.
Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya wenyeji Oljoro JKT na Yanga.
Mtibwa Sugar itacheza na Ruvu Shooting (Uwanja wa Manungu, Morogoro), Mgambo Shooting na Kagera Sugar zitaoneshana kazi kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga huku Mbeya City ikiumana na Azam kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Simba na Ashanti United zitapambana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment