BUKOBA SPORTS

Friday, April 11, 2014

AZAM FC KUTANGAZA UBINGWA MBEYA JUMAPILI? BADO POINTI 3 TU!

Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaendelea (Aprili 12 mwaka huu) na tarehe 13 Jumapili.
Kesho kutwa (Aprili 13 mwaka huu) kutakuwa na mechi nyingine tano za kukamilisha raundi hiyo. 

Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya wenyeji Oljoro JKT na Yanga.
Mtibwa Sugar itacheza na Ruvu Shooting (Uwanja wa Manungu, Morogoro), Mgambo Shooting na Kagera Sugar zitaoneshana kazi kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga huku Mbeya City ikiumana na Azam kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Mtanange wa kukata na Shoka wa kumalizia msimu kwa upande wa timu ya Azam FC ambayo ipo kileleniMbeya City wakichinja chinja hapa!! ikiwa ni moja ya staili yao ya kushangilia baada ya kuifunga timu

No comments:

Post a Comment