BUKOBA SPORTS

Tuesday, April 29, 2014

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: USIKU HUU NI PATASHIKA!! BAYERN MUNICH vs REAL MADRID

FC Bayern Munich v Real Madrid CF
Allianz Arena, Munich, Germany

Rekodi ya Bayern Munich wakiwa Nyumbani kwao dhidi ya Real Madrid ni Ushindi: 8, Sare: 1 Kufungwa: 0. Real Madrid wameshinda mara 2 tu katika safari zao 27 Nchini Germany, mojawapo ikiwa ni ushindi wa Bao 6-1 dhidi ya FC Schalke katika Raundi ya Mtoano ya Timu 16 Msimu huu. 

Bayern wamefanikiwa kupindua vipigo vya Mechi za Kwanza za Ulaya za Ugenini mara 9 kwa kushinda kwao, lakini wamefungwa mara 10 zikiwemo mara 7 katika Mechi zao 9 walizocheza mwisho na kuanza kufungwa Ugenini 
Katika Mechi 6 ambazo walifungwa Bao 1-0 Ugenini, Bayern wameweza kushinda Mechi 5 na ya mwisho ilikuwa Msimu wa 2011/12 walipofungwa na FC Basel kwenye Raundi ya Mtoano ya Timu 16 na kuweza kuwatwanga 7-0 katika Marudiano Mjini Munich. 
Real Madrid wameweza kufuzu mara 43 kati ya 56 ambazo walitangulia kushinda Nyumbani kwao.
Waliposhinda 1-0 Uwanjani Santiago Bernabéu, Real wameweza kushinda mara 4 kati ya 6 na mara hizo mbili walizotolewa kwenye Marudiano ilikuwa dhidi ya Juventus, Misimu ya 2004/05 na 1995/96, na marazote walichapwa 2-0 kwenye Marudiano.

No comments:

Post a Comment