BUKOBA SPORTS

Tuesday, April 29, 2014

WACHEZAJI WA CHELSEA MAZOEZINI KUJIWEKA FITI MTANANGE WA UEFA CHAMPIONS LEAGUE MARUDIANO NA ATLETICO MADRID.... Petr Cech, John Terry, Eden Hazard na Samuel Eto'o ndani...

Kipa Schwarzer akipasha hapa tayari kwa mchezo wa kesho jumatano na Atletico MadridJohn TerryKocha Jose Mourinho akiangalia vijana wakeKipa Petr Cech ndani na kapona...Kazi ipo kesho kwenye marudianoKatika Mashindano ya UEFA, Chelsea wamefungwa mara 2 tu kati ya 7 ambazo walitoka Sare Ugenini. Wakitoka Sare 0-0 Ugenini, Chelsea wameshinda mara 1 tu na kufungwa mara 2 na hivi karibuni ni pale walipotolewa na Barcelona kwenye Nusu Fainali ya 2008/09 walipotoka 0-0 huko Nou Camp na kufungana 1-1 Stamford Bridge.

Chelsea wameshinda mara 1 tu kati ya 4 walizokutana Nusu Fainali na Klabu toka Spain na hiyo moja ilikuwa dhidi ya Barcelona Msimu wa 2011/12. Mwaka 2009 walitolewa na Barcelona, 1998/99 walitolewa na RCD Mallorca kwenye Kombe la Washindi la UEFA na 1994/95, walibwagwa na Real Zaragoza.

Atletico, ambao wamefuzu mara zote mbili baada kutoka Sare 0-0 Nyumbani, wameshinda mara 1 tu Ugenini dhidi ya Klabu za England kati ya Mechi 9. Mara hiyo 1 ni pale walipoifunga Leicester City FC Msimu wa 1997/98 kwenye Raundi ya Kwanza ya UEFA Cup.John Terry kwenye mazoezi na Cesar Azpilicueta, Gary Cahill, Frank Lampard pamoja na Tomas Kalas

No comments:

Post a Comment