BUKOBA SPORTS

Monday, April 28, 2014

ARSENAL 3 v NEWCASTLE 0, GUNNERS WAFANYA KWELI EMIRATES! KOCHA PARDEW KIBARUA KUOTA NYASI!!!

Arsenal leo wameonesha nia ya kubaki top 4 baada ya kuifunga Newcastle bao 3-0, Bao za Arsenal zilifungwa kipindi cha kwanza mbili na moja kipindi cha pili.
Dakika ya 26 Laurent Koscielny aliipachikia bao Arsenal baada ya Santi Cazorla kupiga frii kiki.
Huku bao la pili likifungwa na Mesut Ozil na kufanya 2-0 dhidi ya Newcastle dakika ya 42.
Bao la tatu na la mwisho limefungwa na Olivier Giroud kipindi cha pili dakika ya 66.Kipigo hiki ni muendelezo wa Matokeo mabaya kwa Newcastle ambao sasa wamefungwa katika Mechi zao 7 kati ya 8 walizocheza mwisho kwenye Ligi na wanabaki kwenye Nafasi yao ya 9.

Olivier Giroud akifunga bao la tatu kwa kichwa na kufanya 3-0 dhidi ya Newcastle
Olivier Giroud akishangilia bao lake.
VIKOSI:
Arsenal:
Szczesny, Sagna, Mertesacker, Koscielny, Monreal, Arteta, Ramsey, Cazorla, Ozil, Podolski, Giroud. 

Subs: Vermaelen, Rosicky, Flamini, Fabianski, Sanogo, Jenkinson, Kallstrom.

Newcastle: Krul, Debuchy, Williamson, Coloccini, Dummett, Tiote, Anita, Sissoko, Gouffran, Gosling, Remy. 

Subs: Yanga-Mbiwa, Haidara, Elliot, Shola Ameobi, Obertan, Steven Taylor, Armstrong.

Referee: Neil Swarbrick

No comments:

Post a Comment