BUKOBA SPORTS

Monday, April 28, 2014

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: KESHO JUMANNE NA JUMATANO - NUSU FAINALI: BAYERN MUNICH vs REAL MADRID, CHELSEA vs ATLETICO MADRID


Bayern Munich v Real Madrid CF
-Allianz Arena, Munich, Germany
-Rekodi ya Bayern Munich wakiwa Nyumbani kwao dhidi ya Real Madrid ni Ushindi: 8, Sare: 1 Kufungwa: 0.

-Real Madrid wameshinda mara 2 tu katika safari zao 27 Nchini Germany, mojawapo ikiwa ni ushindi wa Bao 6-1 dhidi ya FC Schalke katika Raundi ya Mtoano ya Timu 16 Msimu huu.

-Bayern wamefanikiwa kupindua vipigo vya Mechi za Kwanza za Ulaya za Ugenini mara 9 kwa kushinda kwao, lakini wamefungwa mara 10 zikiwemo mara 7 katika Mechi zao 9 walizocheza mwisho na kuanza kufungwa Ugenini

-Katika Mechi 6 ambazo walifungwa Bao 1-0 Ugenini, Bayern wameweza kushinda Mechi 5 na ya mwisho ilikuwa Msimu wa 2011/12 walipofungwa na FC Basel kwenye Raundi ya Mtoano ya Timu 16 na kuweza kuwatwanga 7-0 katika Marudiano Mjini Munich.

-Real Madrid wameweza kufuzu mara 43 kati ya 56 ambazo walitangulia kushinda Nyumbani kwao.

-Waliposhinda 1-0 Uwanjani Santiago Bernabéu, Real wameweza kushinda mara 4 kati ya 6 na mara hizo mbili walizotolewa kwenye Marudiano ilikuwa dhidi ya Juventus, Misimu ya 2004/05 na 1995/96, na mara zote walichapwa 2-0 kwenye Marudiano.

Chelsea FC v Atlético Madrid

-Stamford Bridge, London, England

-Katika Mashindano ya UEFA, Chelsea wamefungwa mara 2 tu kati ya 7 ambazo walitoka Sare Ugenini.

-Wakitoka Sare 0-0 Ugenini, Chelsea wameshinda mara 1 tu na kufungwa mara 2 na hivi karibuni ni pale walipotolewa na Barcelona kwenye Nusu Fainali ya 2008/09 walipotoka 0-0 huko Nou Camp na kufungana 1-1 Stamford Bridge.

-Chelsea wameshinda mara 1 tu kati ya 4 walizokutana Nusu Fainali na Klabu toka Spain na hiyo moja ilikuwa dhidi ya Barcelona Msimu wa 2011/12. Mwaka 2009 walitolewa na Barcelona, 1998/99 walitolewa na RCD Mallorca kwenye Kombe la Washindi la UEFA na 1994/95, walibwagwa na Real Zaragoza.

-Atletico, ambao wamefuzu mara zote mbili baada kutoka Sare 0-0 Nyumbani, wameshinda mara 1 tu Ugenini dhidi ya Klabu za England kati ya Mechi 9. Mara hiyo 1 ni pale walipoifunga Leicester City FC Msimu wa 1997/98 kwenye Raundi ya Kwanza ya UEFA Cup.

UEFA CHAMPIONS LEAGUE
NUSU FAINALI:

Marudiano
[Mechi zote Saa 3 Dakika 45 Usiku]
Jumanne Aprili 29

Bayern Munich v Real Madrid [0-1]
Jumatano Aprili 30
Chelsea v Atletico Madrid [0-0]


DONDOO MUHIMU:
FAINALI: Estádio da Luz, Lisbon, Portugal 24 Mei 2014
Bayern Munich/Real Madrid v Chelsea/Atletico Madrid

No comments:

Post a Comment