BUKOBA SPORTS

Tuesday, April 1, 2014

VURUGU ZILIZOTOKEA MECHI YA KAGERA SUGAR NA RUVU SHOOTING, KRFA WAMEJIPANGAJE KWENYE MECHI YA KAGERA SUGAR NA SIMBA JUMAMOSI 5-4-2014 KAITABA?


Kijana wa Kimasai alisababisha vurugu, Wadau wa soka walioshuhudia kwa karibu tukio zima walidai kuwa huyo kijana wa kimasai alikuwa kalewa kwani alikuwa hata akiwapiga Wamasai wenzake na hapo juu ni baada ya kudhibitiwa na Polisi wa Ulinzi kwenye Uwanja huo wa Kaitaba Jumapili kwenye Mtanange Kagera Sugar na Ruvu Shooting, Mtanange uliomalizika kwa Sare ya bila kufungana kwa 0-0.
Wakati zikiwa zimesalia siku chache kufanyika mtanange mkali wa Kagera Sugar na Simba ligi kuu vadacom katika uwanja wa Kaitaba siku ya Jumamosi 5-4-2014 chama cha mpira Mkoa wa Kagera kimejipangaje kuhakikisha kinathibiti vurugu zinazoweza kutokea na kusababisha kuhatarisha usalama wa mashabiki, Katika mechi ya Kagera Sugar na Ruvu Shooting iliyochezwa jumapili 30-3-2014. Tumeshuhudia vurugu zilizozukiwa na Kijana mmoja wa kimasai aliemvamia shabiki mmoja alietambulika kwa jina la Moses Nyama ambae ni msanii katika bend ya muziki ya Kakau kumpiga akishilikiana na wenzake kwa fimbo huku wakiwa na siraha za visu viunoni na kumjerui kabla ya mashabiki kuingilia kati kumnusuru na badae Polisi kufika wakiwa wakitazama mpira badala ya usalama wa raia. Ili kudhibiti hali hii ya mashabiki kuingia uwanjani na fimbo, visu, mikuki nk. KRFA na Jeshi la Polisi mmejipanga vipi katika mtanange wa Kagera Sugar na Simba Jumamosi 5-4-2014 ?
Kijana wa Kimasai akiendelea kuwapa hali ngumu hata waliomshika kumzuia!!
Tulia we kijana!!
Huyu ni Mmasai ambaye ni miongoni mwa waliojerui akiwa na sime kiunoni akizibitiwa na Askari waliovaa kiraia.

Mmasai akiwa kapandisha mzuka anataka kupiga mtu na wengine wakiwa wamedhibitiwa na Mashabiki

Wote hawa Wamasai walivamia mtu mmoja kwa fimbo zao na kumjeruhi.
Mwenye kaunda suti ni Katibu wa KRFA Salumu Chama alilazimika kuingilia kati sakata hili

Baada ya dakika kadhaa Polisi waliokuwa wakiangalia mpira walikuja baada ya mashabiki kupiga kelele. Na hapa ndipo swala la kujiuliza na kufanyiwa kazi, je Polisi anapoingia uwanjani ni kwa ajili ya kuangalia mpira au usalama wa mashabiki? swali kwa wahusika.
Je kuingia na fimbo na visu uwanjani ni sahihi? Wote mmepewa kazi kwenye uwanja wa Kaitaba?
Chini ya ulinzi mkali wa Polisi

Kiongozi KRFA Chama akiwatuliza!!!




Mmasai akiwa tayari kapigwa pingu tayari kwenda kituoni
Chezea askari wewe!!!

Alichukuliwa na Gari la police na kupelekwa kituoni
Mpira wa Kagera Sugar V Ruvu Shooting ulikuwa ukiendelea kama kawaida 

No comments:

Post a Comment