BUKOBA SPORTS

Tuesday, April 1, 2014

FULL TIME: UEFA CHAMPIONS LEAGUE- MANCHESTER UNITED 1 v BAYERN MUNICH 1, HAKUNA MBABE!! NGOMA YAMALIZIKA KWA SARE!

Rio Ferdinand akimpongeza Nemanja Vidic baada ya kuifungia Man United bao kwa kichwa kipindi cha pili kwenye uwanja wa Old Trafford.Vidic akijitwisha ndoo na kufungaBao....1-01-1, Bastian Schweinsteiger aliwasawazishia bao BayernDanny Welbeck akiwapelekesha mabeki wa Bayern Munich usiku huuKaribu sana hapa kwetu Old Trafford, Meneja David Moyes akisalimiana na kocha wa Bayern MunichMpira ni mapumziko, Si United wala Bayern..Wote ni 0-0 ndani ya Uwanja wa Old Trafford. 
Kipindi cha pili kimeanza......Kipindi cha pili dakika ya 58 United  wanapata bao baada ya kupigwa kona mfungaji ni Nemanja Vidic kona ikipigwa na Wayne Rooney. Dakika ya 66 Bastian Schweinsteiger aliisawazishia bao Bayern Munich kwa kufanya 1-1 baada ya kupata pasi kutoka kwa Mario Mandzukic. Dakika ya 90 mchezaji wa Bayern Munich  Bastian Schweinsteiger anapewa kadi nyekundu baada ya kumwangusha Wayne Rooney. Danny Welbeck alipata nafasi lakini hakuweza kuitumia vyema kipindi cha kwanza mwishoni.
Bastian Schweinsteiger akishangilia bao lake la kusawazisha kipindi cha piliNa kadi ya njano juuView image on TwitterMashabiki wa Bayern MunichSir Alex Ferguson akiweka mambo sawa kwenye saa yake, Old Trafford View image on TwitterBaadhi ya wachezaji wa Manchester United wakiingia uwanjani Old Trafford

VIKOSI:
Manchester United starting XI
De Gea, Jones, Ferdinand, Vidic, Buttner, Valencia, Carrick, Fellaini, Giggs, Rooney, Welbeck.

Bayern Munich starting XI
Neuer, Rafinha, Boateng, Martinez, Alaba, Robben, Lahm, Schweinsteiger, Kroos, Muller, Ribery.

No comments:

Post a Comment