Miongoni mwa Mechi hizo 4 ni ile itakayochezwa huko Stade de Gerland, Jijini Lyon wakati Wenyeji Olympique Lyonnais itakapowakaribisha Vigogo wa Italy Juventus.
Huko Nchini Netherlands, kwenye Mji wa Alkmaar, AZ Alkmaar, watakuwa kwao Stadium Alkmaarderhout kucheza na Benfica ya Portugal na huko Mjini Basel, Uswisi, FC Basel 1893 itakairibisha Klabu ya Spain, Valencia, Uwanjani St. Jakob Park.
Ndani ya Uwanja maarufu, Estadio do Dragao huko Jijini Porto, Ureno, FC Porto watacheza na Sevilla ya Spain.
Mechi zote hizo zitaanza Saa 4 Dakika 5 Usiku, kwa Saa za Bongo.
Timu hizi zitarudiana Alhamisi Aprili 10.
EUROPA LEAGUE
Robo Fainali
[Mechi zote kuanza Saa 4 Dakika 5 Usiku]
Alhamisi Aprili 3
AZ Alkmaar - Netherlands v Benfica - Portugal [Stadium Alkmaarderhout]
FC Basel 1893 – Switzerland v Valencia - Spain [St. Jakob Park]
FC Porto – Portugal v Sevilla FC – Spain [Estadio do Dragao]
Olympique Lyonnais – France v Juventus FC – Italy [Stade de Gerland]
Marudiano
Alhamisi Aprili 10
Juventus FC – Italy v Olympique Lyonnais – France [Juventus Arena]
Valencia – Spain v FC Basel 1893 - Switzerland [Estadio Mestalla]
Sevilla FC – Spain v FC Porto – Portugal [Estadio Ramon Sanchez Pizjuan]
Benfica – Portugal v AZ Alkmaar – Netherlands [Estadio da Luz]
SAFARI YA TURIN
NUSU FAINALI: Droo Aprili 11, Mechi Aprili 24 na Mei 1
FAINALI: Jumatano Mei 14, Juventus Stadium, Turin, Italy
No comments:
Post a Comment