BUKOBA SPORTS

Tuesday, April 1, 2014

ROBO FAINALI CHAMPIONS LEAGUE: USIKU HUU - MAN UNITED vs BAYERN MUNICH, BARCELONA VS ATLETICO MADRID


Nani wa kumzuia Ribery hasifanye kile anachotaka kukifanya?Rafael kuukosa mtanange huu, Bado anauguza majeraha!

Manchester United vs Bayern Munich

Barcelona vs Atletico Madrid
Kwenye La Liga, Atletico ndio Vinara na Barca wako nyuma yao kwa Pointi 1 na Msimu huu wameshakutana mara 3 na mara zote ni suluhu ingawa Barca walizoa Supercopa de Espana Mwezi Agosti kwa Bao la Ugenini baada ya Sare ya Mechi zote mbili.
Licha ya kulingana nguvu Msimu huu, Barca ndio wazoefu kwa Mechi za Ulaya na wameweza kufika Nusu Fainali za UCL katika Misimu 6 iliyopita wakati Atletico wako kwenye Robo Fainali yao ya kwanza tangu Mwaka 1997 na hawajatinga Nusu Fainali ya Michuano hii ya Ulaya kwa Miaka 40.

Mara ya mwisho kwa Atletico kufika Robo Fainali ya Michuano hii, Miaka 17 iliyopita, Kocha wao wa sasa, Diego Simeone, alikuwemo kwenye Kikosi kilichotolewa kwa Jumla ya Bao 4-3 na Ajax.
Pia, Atletico hawajawahi kushinda Uwanjani Nou Camp tangu Mwaka 2006 waliposhinda 3-1 kwenye La Liga na Fernando Torres, ambae sasa yuko Chelsea, kufunga Bao 2.

Hata hivyo, Rekodi ya Barca dhidi ya Klabu nyingine ya Spain kwenye michuano ya Ulaya si nzuri baada kupoteza mara 5 kati ya 9 lakini wamefungwa Mechi 1 tu kati ya 26 za Ulaya walizocheza mwisho Uwanjani kwao Nou Camp.
Kila Timu itatinga kwenye Mechi hii ikiwakosa baadhi ya Wachezaji wao na Barca watamkosa Kipa wao, Victor Valdes, ambae aliumia Goti hivi Juzi na atakuwa nje kwa Miezi 7.
Atletico itacheza bila ya Majeruhi Javier Manquillo na Raul Garcia ambae amefungiwa.

No comments:

Post a Comment