Ngorongoro Heroes inayofundishwa na John Simkoko ipo kambini tangu Machi 23 mwaka huu kujiandaa kwa mechi dhidi ya Kenya (U20). Mechi hiyo ya michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri huo itachezwa Jumapili (Aprili 6 mwaka huu) saa 10 kamili jioni Uwanja wa Machakos ulioko kilometa 80 kutoka jijini Nairobi.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo (Aprili 1 mwaka huu), Kocha Simkoko amesema wachezaji wake wapo tayari kwa ajili ya mechi hiyo, na nia ni kupata matokeo mazuri kabla ya mchezo wa marudiano utakaochezwa nchini wiki tatu baadaye.

Ngorongoro Heroes itaagwa kesho (Aprili 2 mwaka huu) saa 5 asubuhi kwenye ofisi za TFF.
MIKOA KUMI YATUMA WAWAKILISHI WAKE RCL
Vyama vya mpira wa miguu vya mikoa kumi vimewasilisha majina ya mabingwa wao watakaoshiriki Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL).
Mabingwa hao ni Arusha (AFC), Kilimanjaro (Panone FC), Lindi (Kariakoo SC), Manyara (Tanzanite SC), Mara (JKT Rwamukoma), Morogoro (Volcano FC), Mtwara (Pachoto Shooting Stars), Pwani (Kiluvya United), Shinyanga (Bulyanhulu FC), Singida (Singida United) na Tanga (African Sports).
Mikoa ambayo haijawasilisha mabingwa wake ni Dar es Salaam, Dodoma, Geita, Iringa, Kagera, Katavi, Kigoma, Mbeya, Morogoro, Njombe, Rukwa, Ruvuma, Simiyu na Tabora wakati mikoa ya Dodoma na Mwanza imeomba kuongezewa muda kutokana na sababu mbalimbali.
Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliagiza kuwa mikoa yote iwe imemaliza ligi na kuwasilisha jina la bingwa wake Machi 30 mwaka huu.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment