BUKOBA SPORTS

Saturday, April 12, 2014

FA CUP: WIGAN 1 vs ARSENAL 1, KIPA FABIANSKI AWABEBA GUNNERS KWENDA FAINALI...BAADA YA KWENDA DAKIKA 120 NA KUDAKA MIKWAJU MIWILI YA PENATI.

Wachezaji wa Arsenal wakimpongeza kipa wao Lukasz Fabianski baada ya kuwasaidia kuokoa mikwaju ya penati na hatimaye timu hiyo kusonga hatua inayofuata ya fainali.Arsenal Leo hii Uwanjani Wembley wamefanikiwa kuwabwaga Mabingwa Watetezi wa FA CUP, Wigan Athletic,kwenye Nusu Fainali kwa Penati 4-2 na wao kutinga Fainali baada Mechi kwenda Dakika 120 Matokeo yakiwa Bao 1-1.
Wigan walikosa Penati zao mbili za kwanza kupitia Caldwell na Collison kwa Kipa Fabianski kuokoa na Arsenal kufunga Penati 4 kupitia Arteta, Kallstrom, Giroud na Cazorla.

Penati za Wigan zilizofungwa zilipigwa na Jean Beausejour na McArthur.
Hadi Mapumziko Bao zilkuwa 0-0 na Wigan ndio waliotangulia kufunga katika Dakika ya 63 kwa Penati ya Gomez ambayo ilitolewa baada ya Mertesacker kumwangusha McManaman.
Arsenal walisawazisha katika Dakika ya 83 kufuatia Kona na piga nikupige kuishia kwa Mertesacker alieukwamisha Mpira wavuni.
Hadi Dakika 90 kumalizika Bao zilikuwa 1-1 na zikaongezwa Dakika 30 za Nyongeza lakini mambo hayakubadilika.

Nusu Fainali nyingine itachezwa kesho Jumapili, pia Uwanjani Wembley, kati ya Hull City na Sheffield United.
Kipa wa Arsenal Lukasz Fabianski akiokoa mikwaju ya penati miwili ya mwanzoKocha Arsene WengerAlex Oxlade-Chamberlain na kipa wa Wigan Scott CarsonKipa wa Arsenal FABIANSKIKocha wa Wigan akiwapa maelekezo vijana wakeMchezaji Mertesacker wa Arsenal akimfanyia rafu McManaman wa WiganPenati...Jordi Gomez akifunga bao kwa mkwaju wa penati na kufanya 1-0Jordi Gomez akishangilia bao lakeKocha Arsene Wenger akipagawa baada ya bao hiloMertesacker alisawazisha na kufanya 1-1

Alex Oxlade-Chamberlain chupuchupu amfunge kipa wa WiganMapema wachezaji wakiwakumbuka wenzao waliopoteza maisha
VIKOSI 
Arsenal: Fabianski, Sagna, Mertesacker, Vermaelen, Monreal, Arteta, Oxlade-Chamberlain, Ramsey, Cazorla, Podolski, Sanogo
Subs: Szczesny, Jenkinson, Gibbs, Kallstrom, Akpom, Eisfeld, Giroud

Wigan: Carson, Perch, Boyce, Ramis, Crainey, McArthur, McEachran, McManaman, Beausejour, Gomez, Fortune
Subs: Al Habsi, Barnett, Caldwell, Maloney, Espinoza, Collison, Powell

No comments:

Post a Comment