BUKOBA SPORTS

Monday, May 5, 2014

BOSI KARL-HEINZ WA BAYERN AWAWAKIA TONI KROOS NA THOMAS MULLER KUTAKA KUKIMBILIA UNITED!! AWATAKA WAWE WAZI NA WAMWAMBIE YEYE!!

Toni Kroos na Thomas Muller wameonywa na Mtendaji Mkuu wa Klabu hiyo Karl-Heinz Rummenigge kwamba wanapaswa kumuona yeye ikiwa wana nia ya kuhamia Manchester United.
Huku minong’ono ikizidi kutanda kuwa Meneja mpya wa Man United Louis van Gaal atatangazwa Wiki hii, pia upo uvumi mzito uliotanda kwamba Kocha huyo wa Timu ya Taifa ya Holland anataka kutua nao Old Trafford Wajerumani hao.
Kroos, Miaka 24, amekuwa akivumishwa sana kwamba yu njiani kuelekea Old Trafford hasa kwa vile amegoma kusaini Mkataba mpya na Bayern wakati wa sasa ukitarajiwa kumalizika mwishoni mwa Msimu ujao.
Nae Thomas Muller, mwenye Miaka 24 na ambae amekuwa akipigwa Benchi na Pep Guardiola tangu ashike wadhifa huo mwanzoni mwa Msimu huu, anataka kung’’oka ili apate namba ya kudumu kwingineko na Man United ikitajwa ndio lengo lake kubwa.
Hata hivyo, Bosi Karl-Heinz Rummenigge, akionyesha kuwachimba mkwala Wachezaji hao, ametishia kwa kuwaambia: “Ikiwa Mchezaji anahisi hajisikii kukaa Bayern Munich lazima aje Ofisini kwangu! Hapo ndio tutazungumza!”

Wakati Muller amekiri bayana na kutofurahishwa na kupigwa Benchi, hasa kwenye Nusu Fainali za UEFA CHAMPIONS LIGI na Real Madrid, Kroos, alipohojiwa kuhusu nia yake kwenda Man United, alijibu: “Sina la kusema!”
Wachezaji wote hao wawili wanatarajiwa kuwemo kwenye Kikosi cha Germany kitakachocheza Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil zinazoanza Juni 12.

No comments:

Post a Comment