BUKOBA SPORTS

Monday, May 5, 2014

BRENDAN ROGERS ASEMA ATAKUFA NA MTU USIKU HUU!!! APANGA KUREJEA KILELENI LIGI KUU ENGLAND NA KUTWAA UBINGWA! LEO JUMATATU WAPO UGENINI NA CRYSTAL PALACE

KOCHA wa Liverpool, Brendan Rodgers bado ana matumaini ya kuchukua ubingwa licha ya kutolewa kileleni na Manchester City. BAADA kucharazwa Bao 2-0 Jumapili iliyopita Uwanjani kwao Anfield na ‘Kikosi cha Pili’ cha Chelsea na kuifungulia njia Manchester City kupanda kileleni, Jumatatu Usiku Liverpool wana nafasi ya kurejea kileleni tena watakapocheza Ugenini na Crystal Palace. 
Liverpool na Man City zote zimefungana kwa Pointi 80 kila mmoja na huku kila Timu imebakisha Mechi mbili lakini City wako juu kwa Ubora wa Tofauti ya Magoli na wamewazidi Liverpool Bao 9.
Hivyo kazi kubwa kwa Liverpool ni kuifunga Palace, tena kuifunga Bao nyingi, ili kuipa presha City ambao wanacheza Jumatano Nyumbani kwao Etihad na Aston Villa. 


Wapinzani wa Liverpool, Crystal Palace, chini ya Meneja mahiri Tony Pulis, wao watacheza Mechi hii bila woga wowote kwani tayari wamejihakikishia kubaki Ligi Kuu England.
Smiles: Brendan Rodgers says his players will have to solve their own frustration problemsVijana wa Manuel Pellegrini walipanda kileleni kwa wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa baada ya kushinda mabao 3-2 dhidi ya Everton kwenye uwanja wa Goodison Park jumamosi iliyopita, huku wakisubiri mechi ya leo baina ya Liverpool na Crystal Palace. 
Kama timu zote zitashinda mechi zao mbili za mwisho, bingwa atapatikana kwa tofauti ya magoli, na Rodgers anaamini timu yake itafunga mabao mengi zaidi katika mechi zake za mwisho ili kujiweka mazingira mazuri ya kubeba taji.
 “Kama kuna timu itakayofunga mabao mengi na kubadili mambo tutakuwa sisi”. Aliwaambia waandishi wa habari. 
“Hakuna swali hapo. Hilo ndio lengo letu. Hakuna swali kuhusu hilo. Nimeona siku za nyuma. Chelsea waliwafunga Wigan 8-0 katika mchezo wa mwisho wa msimu (kipindi Chelsea walipotwaa ubingwa mwaka 2010).

“Siwadharau hata kidogo Newcastle, lakini kama kuna timu yoyote iliyoonesha uwezo wa kufunga magoli, ni sisi. Sisi sio watu wa 1-0. Tulionesha hilo mwanzoni mwa msimu, lakini tulichokionesha tangu mwanzoni ni kwamba tunao uwezo wa kufunga magoli mengi”. Aliongeza Rodgers. 

City wanajiombea ushindi katika mechi zao mbili za mwisho dhidi ya Aston Villa na West Ham, zote zitapigwa Etihad, lakini Rodgers anaamini hawatazoa pointi zote sita.
“Ni kazi ngumu kwa City,” Aliongeza. “Aston Villa ni timu bora, tena inayoshambulia kwa kushitukiza na wanakuwa wazuri zaidi wanapokuwa ugenini, na West Ham siku hiyo watatoa upinzani mkubwa”.



LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
Jumatatu 5 Mei 2014

22:00 Crystal Palace v Liverpool

Jumanne 6 Mei 2014
21:45 Man United v Hull
Jumatano 7 Mei 2014
21:45 Man City v Aston Villa
21:45 Sunderland v West Brom


No comments:

Post a Comment