BUKOBA SPORTS

Tuesday, May 13, 2014

EUROPA LIGI - FAINALI JUMATANO: BENFICA v SEVILLA!

BENFICA, watajaribu kwa mara ya 9, kuifuta ‘LAANA’ ya Lejendari Meneja wao wa zamani Bela Guttman ambae aliiongoza Klabu hiyo kubwa Ureno kati ya 1959 na 1962, watakapocheza Fainali ya EUROPA LIGI na Sevilla ya Spain.
Bela Guttman, ambae ndie alimsaini Lejendari wa Ureno Eusebio, aliipa Benfica Mataji kadhaa ya Nchini Ureno na Mawili ya Ulaya, lakini aliondoka Klabu hiyo kwa ugomvi mkubwa kutokana na mvutano wa Malipo yake na kuilaani Benfica kwa kutamka haitatwaa Taji lolote Ulaya kwa Miaka 100.
Tangu wakati huo Benfica wameshashindwa Fainali 8 za Ulaya ikiwemo ile ya Kombe la Ulaya la Mwaka 1988 walipofungwa kwa Penati na PSV na Msimu uliopita kutolewa na Chelsea kwenye Fainali ya EUROPA LIGI huku Bao la ushindi la Chelsea likifungwa Dakika ya 93 na Branislav Ivanovic.

No comments:

Post a Comment