Kwenye Fainali hiyo, QPR itakutana na
Derby County ambayo Juzi iliibwaga Brighton Jumla ya Bao 6-2 katika
Mechji mbili baada kuichapa 4-1 kwenye Mechi ya Pili.
Mechi hizi za Mchujo za Klabu za Daraja
la Championship huko England zinahusisha Klabu zilizomaliza Nafasi za 3
hadi 6 kusaka Timu moja kuungana na Mabingwa wa Daraja hilo, Leicester
City, pamoja na Timu ya Pili, Burnley, kucheza Ligi Kuu England Msimu
ujao.
QPR na Wigan zilitoka Sare ya 0-0 katika Mechi ya Kwanza.
Wigan walitangulia kufunga katika Dakika
ya 9 na QPR, chini ya Meneja Mkongwe Harry Redknapp, ilisawazisha
Kipindi cha Pili kwa Penati ya Austin ambayo ilitolewa na Refa Mark
Clattenburg baada Gary Caldwell kumwangusha Hoilett.
Bao la ushindi la QPR lilifungwa tena na Austin katika Kipindi cha Kwanza cha Dakika za Nyongeza 30, kwenye Dakika ya 96.
QPR na Derby County zitacheza Fainali
Uwanjani Wembley hapo Mei 24 kupata Timu moja nay a 3 kupanda Daraja
kucheza Ligi Kuu England Msimu ujao.
RATIBA/MATOKEO:
Mechi za Pili
[Kwenye Mabano Jumla ya Mabao kwa Mechi mbili]
Jumapili Mei 11
Derby County 4 Brighton and Hove Albion 1 [6-2]
Jumatatu Mei 12.
Queens Park Rangers 2 Wigan Athletic 1 [2-1]
Jumamosi Mei 24
17:00 Fainali - Wembley Stadium
Derby County vs QPR
No comments:
Post a Comment