KALENDA MSIMU WA SOKA ENGLAND 2014/15 YATOKA! NGAO YA JAMII WIKIENDI AGOSTI 9/10, LIGI KUU ENGLAND KUANZA AGOSTI 16
KALENDA ya Msimu wa Soka wa England wa 2014/15 imetangazwa na Ligi Kuu England itaanza rasmi Agosti 16.
Zile Tarehe muhimu za Msimu wote huo mpya zimeanikwa ikiwa ni pamoja na FA CUP, CAPITAL ONE CUP pamoja na Mechi za Mashindano ya Ulaya.
Kutokana na kuwepo kwa Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil kuanzia Juni 12 hadi Julai 13, Msimu wa 2014/15 utachelewa kidogo kuanza kwa Ligi Kuu England kuanza Agosti 16 na kumalizika Mwakani Mei 24.
Ligi za Madaraja ya chini ya Ligi Kuu England zitaanza Wiki moja kabla ya Ligi Kuu England na lile pambano la Kufungua Pazia Msimu mpya, kugombea Ngao ya Jamii, litachezwa Uwanja wa Wembley Wikiendi ya Agosti 9/10.
Raundi ya Kwanza ya CAPITAL ONE CUP, inayoshirikisha Klabu za Madaraja kwenye Raundi hiyo, itaanza kuchezwa Kati-Wiki ya Agosti 12 na 13 huku Fainali ikichezwa Uwanja wa Wembley Jumapili Machi 1, 2015.
Nusu Fainali za FA CUP zitachezwa Wikiendi ya Aprili 18 na 19, 2015 na Fainali ni Uwanja wa Wembley Mei 30,2015.
Vile vile Mechi za Timu ya Taifa ya England za kufuzu kucheza EURO 2016 huko France zipo kwenye Kalenda hiyo na Mechi yao ya kwanza ni Ugenini na Switzerland kwenye Wiki inayoanzia Septemba 8.
Pia, Mechi za Awali za Mtoano za UEFA CHAMPIONS LIGI na EUROPA LIGI zimo na Arsenal, ikiwa watamaliza Nafasi ya 4 kwenye Ligi Kuu England kama inavyotarajiwa, wataanza Kampeni yao ya UEFA CHAMPIONs LIGI, Msimu wa 2014/15, Raundi ya Mtoano, hapo 29/30 Julai 2014.
TAREHE MUHIMU:
-NGAO ya JAMII=Kuchezwa Wikiendi ya Agosti 9 na 10
-LIGI KUU ENGLAND=Kuanza Agosti 16, Kumalizika 24 Mei 2015
-CAPITAL ONE CUP=Fainali 1 Machi 2015
-FA CUP=Nusu Fainal Wikiendi ya 18/19 Aprili 2015, Fainali ni Wembley Mei 30,2015
-UEFA CHAMPIONS LIGI=Arsenal, wakimaliza Nafasi ya 4 kwenye Ligi Kuu England, wataanza Kampeni yao ya UEFA CHAMPIONS LIGI, Msimu wa 2014/15, Raundi ya Mtoano, hapo 29/30 Julai 2014
No comments:
Post a Comment