BUKOBA SPORTS

Sunday, May 11, 2014

MHE. NYALANDU AKABIDHIWA MAGARI YA KUSAIDIA KAMPENI YA KUTOKOMEZA MAJANGILI WA MAUAJI YA TEMBO


Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nayalandu, akionyesha funguo ya moja kati ya magari matatu aina ya Land Cruiser, yenye thamani ya Sh. milioni 350, baada ya kupokea kutoka kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Uhifadhi Wanyamapori Tanzania, Eric Pasanisi (kulia) wakati wa hafla ya makabidhiano hayo iliyofanyika jana kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro wakati wa Kongamano la Kampeni ya kudhibiti Ujangili na kukomesha mauaji dhidi ya Tembo, Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, Abdulkarim Shah.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nayalandu, akijaribu kuwasha moja kati ya magari matatu aina ya Land Cruiser, yenye thamani ya Sh. milioni 350, baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa Taasisi ya Uhifadhi Wanyamapori Tanzania, Eric Pasanisi, wakati wa hafla ya makabidhiano hayo iliyofanyika jana kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro wakati wa Kongamano la Kampeni ya kudhibiti Ujangili na kukomesha mauaji dhidi ya Tembo.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nayalandu, akisainiana mkataba wa makabidhiano wa magari matatu aina ya Land Cruiser, yenye thamani ya Sh. milioni 350, na Mwenyekiti wa Taasisi ya Uhifadhi Wanyamapori Tanzania, Eric Pasanisi (wa pili kushoto) wakati wa hafla ya makabidhiano hayo iliyofanyika jana kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro wakati wa Kongamano la Kampeni ya kudhibiti Ujangili na kukomesha mauaji dhidi ya Tembo, kushoto ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhri, Job Ndugai (kulia) ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mahmoud Mgimwa.

Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Kampeni ya kudhibiti Ujangili na kukomesha mauaji dhidi ya Tembo, wakiwa katika Kongamano hilo, lililomalizika jan kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro, jijini Dar Es Salaam.

Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dkt. Reginald Mengi, akichangia mada wakati wa Kongamano hilo, lililomalizika jana kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro, Jijini Dar es Salaam.Kongamano hilo lilifunguliwa na Makamu wa Rais Dtk. Mohamed Gharib Bilal.

No comments:

Post a Comment