
Zaidi ya Simba watatu wakiwa wanamkimbiza Nyati huyo mmoja

Simba wawili kati ya watano wakiwa wanajaribu kumuangusha chini Nyati huyu katika mbuga ya wanyama ya Serengeti nchini Tanzania.

Simba mmoja nyuma akiendelea kupambana na Nyati huyu kwa nyuma, huku simba wengine watatu wakiwa mbele yake.

Simba hawa wakiwa wanafanya jitihada zao zote kumuangusha chini bila mafanikio Nyati huyu huku wakiwa wamemuachia alama nyingi za meno na kucha mwilini mwake.

Watalii wanaofika kutembelea vivutio vya utalii Tanzania, wakiangalia shughuli nzito ya Nyati mmoja kuwatoa jasho zaidi ya simba sita katika mbuga ya Serengeti, Simba hao walikuwa wanataka kumuangusha chini na kumfanya kitoweo chao.

TUSIAIBIKE MBELE YA WATALII, HUYU WETU!! Simba zaidi ya sita wakiendelea kumshambulia Nyati mmoja ili wamuangushe chini bila ya mafanikio. Hii imetokea katika mbuga ya wanyama ya Serengeti, Tanzania.

TUMECHEMSHA!!! Simba mmoja kati ya sita akiwa anahema kwa fujo pembeni baada ya kushindwa kumwangusha chini Nyati huyu ambaye ilibidi wamuachie huru baada ya kuvutana naye kwa zaidi ya dakika 20. Nyati huyo baadaye aliondoka zake japo alikuwa na majeraha mengi ya kucha na meno mwilini mwake.
You might also like:
No comments:
Post a Comment