BUKOBA SPORTS

Monday, May 5, 2014

MTAALAMU WA NYASI BANDIA AWASILI, UWANJA WA KAITABA BUKOBA MJINI KUOTA NYASI!!!

Mtaalamu wa nyasi bandia kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Ian McClemen amewasili nchini leo alfajiri (Mei 4 mwaka huu) ambapo atakuwepo kwa siku tatu.

McClemen ameondoka leo (Mei 4 mwak huu) kwenda Bukoba ambapo atakagua Uwanja wa Kaitaba, na kesho (Mei 5 mwaka huu) atakwenda jijini Mwanza kukagua Uwanja wa Nyamagana.

Viwanja hivyo vinawekwa nyasi bandia kwa ufadhili wa FIFA chini ya mpango wa misaada wa Goal Projects. Baada ya ukaguzi huo, McClemen atatuma ripoti yake FIFA ili shirikisho hilo liweze kuteua mkandarasi wa kufanya kazi hiyo.

Kwa Tanzania viwanja vilivyowekwa nyasi bandia hadi sasa kupitia Goal Project ni Uwanja wa Uhuru uliopo Dar es Salaam, Uwanja wa Karume (Dar es Salaam) na Uwanja wa Gombani uliopo Pemba.

Mfano wa Nyasi Bandia.Mkeka wa Nyasi Bandia na Kaitaba kuoneka hivi!!Taswaira ya Uwanja wa Kaitaba kwa sasa
Mkata nyasi sasa kazi yake kwishnei!!!  uwanja wa Kaitaba

Hivi ndivyo uwanja wa Kaitaba ulivyo wakiwa wanaufanyia Usafi. Ikiwa ni pamoja na kukata nyasi zake ambapo mpango uliopo kwa sasa ni kuuwekea nyasi za bandia!!
Nyasi za sasa za Uwanja wa Kaitaba

Willy Kiroyera akiwa kwenye Uwanja wa Kaitaba
Taswira ya uwanja wa Kaitaba kwa sasa

No comments:

Post a Comment