
Tayari Nahodha Nemanja Vidic, ambae nae Mkataba wake unamalizika mwishoni mwa Msimu huu, ameshathibitisha kuhamia Inter Milan ya Italy lakini Giggs anataka Rio na Evra wabakishwe Klabuni hapo.

Giggs amesema: “Naamini bado wana nafasi ya kucheza Msimu ujao. Wako fiti na Wiki iliyopita walicheza vizuri tu! Nimetoa maoni yangu kwa Uongozi na uamuzi utafanywa na wote- Rio, Patrice, Ed Woodward na huyo Meneja mpya!”

No comments:
Post a Comment