BUKOBA SPORTS

Monday, May 12, 2014

SERIE A: BINGWA JUVE WAICHAPA AS ROMA KWAO BAO 1-0, SASA WAWANIA REKODI KUFIKISHA POINTI 100!!


MABINGWA wapya wa Serie A huko Italy, Juventus, ambao Wiki iliyopita walitetea vyema Taji lao wakiwa na Mechi 3 mkononi, Leo wamewachapa wapinzani wao wa karibu waliokuwa wakiwafukuza kwa muda mrefu, AS Roma, waliokuwa kwao Stadio Olimpico, Bao 1-0 kwa Bao la Dakika ya 90 la Daniel Osvaldo.
Osvaldo, Mchezaji wa zamani wa AS Roma, alimalizia kazi njema ya Pogba na ; Lichtsteiner.
Juve, wakiwa wamebakisha Mechi 1 kumaliza Ligi, wanasaka kuwa Klabu ya Kwanza kufikisha Pointi 100 katika Msimu mmoja.

Ligi hii ya Italy itamalizika Wikiendi ijayo na Juve watakuwa Nyumbani kwao Jijini Turin kucheza na Cagliari Calcio. 

MSIMAMO ULIVYO TIMU ZA JUU 4
NA
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
1
Juventus FC
37
32
3
2
77
23
54
99
2
AS Roma
37
26
7
4
72
24
48
85
3
SSC Napoli
37
22
9
6
72
38
34
75
4
ACF Fiorentina
37
19
7
11
63
42
21
64

No comments:

Post a Comment